Klabu ya Leicester City ambayo ipo chini ya kocha mkuu Brendan Rodgers imeshinda mchezo wake wa ligi kuu ya Uingereza hapo jana kwa mara ya kwanza baada ya kucheza michezo saba ila kupata ushindi wowote.

 

Leicester City Yashinda kwa Mara ya Kwanza EPL

Leicester iliitandika Nottingham Forest mabao 4-0 katika uwanja wao wa nyumbani, huku mabao hayo yakitupiwa nyavuni na Harvey Barnes, Patson Daka, pamoja na James Maddison akitupia mawili.

Timu hiyo ya Brendan Rodgers imekuwa ikipitia wakati mgumu toka msimu huu uanze huku presha ikionekana kuwa kubwa kwa kocha huyo, ambae alikuwa na hofu ya kufutwa kazi, lakini timu hiyo akaonyesha imani nae na kuendelea kumuamini abaki klabuni hapo.

Rogers alisema kuwa atakubaliana na lolote ambalo klabu itaamua kutokana na kupata matokeo mabovu ambayo toka timu hiyo ipande daraja haijawahi kupata. Hivyo basi aliamua kukubaliana na maamuzi yoyote ambayo yangefanywa na bodi.

Leicester City Yashinda kwa Mara ya Kwanza EPL

Mechi ya wikiendi ijayo, Leicester atamfuata AFC Bournemouth nyumbani kwake kutafuta alama nyingine tatu ili kujiondoa kwenye nafasi mbaya aliyopo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa