Polisi mkuu na Maafisa 9 nchini Indonesia wamefukuzwa kazi kufuatia  mashabiki takribani 125 kufariki wikiendi hii, kwenye mchezo kati ya Arema dhidi ya Persebaya kutokana na vurugu iliyotokea uwanjani hapo ambapo Arema walipoteza kwa 3-2 dhidi ya Persebaya.

 

Polisi Mkuu na Maafisa 9 Wafukuzwa Kazi Indonesia.

Hilo limekuja baada ya Waziri wa michezo nchini hapo kusema kuwa atukio hilo litafanyiwa uchunguzi wa kina halafu watakuja na majibu. Takriban watu 125 waliuawa katika ghasia zilizotokea kwenye mechi ya soka nchini Indonesia.

Maelfu ya mashabiki wa Arema walivamia uwanjani na kuwarushia chupa na makombora mengine wachezaji na maafisa wa soka baada ya timu yao kushindwa kwa mara ya kwanza nyumbani na klabu pinzani ambayo ni Persebaya katika kipindi cha miaka 23, na kusababisha mapigano na matumizi ya kemikali ya kudhibiti umati iliyopigwa marufuku na FIFA.

Polisi Mkuu na Maafisa 9 Wafukuzwa Kazi Indonesia.

Shirikisho la Soka nchini humo lilisema pia, linaweza kuwapiga marufuku mashabiki kuingia uwanjani kutokana na vurugu ambazo wameleta na kusababisha vifo vya watu wengi siku ya Jumamosi.

Taarifa zinasema kuwa maafisa wengine 18 wa polisi wanaendelea kuchunguzwa kutokana na kusababisha mauaji wa raia hiyo huku wananchi wakiendelea kuwazika marehemu.

Polisi Mkuu na Maafisa 9 Wafukuzwa Kazi Indonesia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa