Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid,Juventus, na Napoli Gonzalo Higuain ametundukia rasmi daluga na kuachana na mpira wa ushindani baada ya kuutumikia kwa muda mrefu.

Gonzalo Higuain amezaliwa 10 Disemba 1987 nchini Argentine, Mshambuliaji huyo alieanza maisha yake ya soka katika klabu ya nyumbani kwao River Plate kabla ya kuhamia klabu ya Real Madrid mwaka 2007.

gonzalo higuainMshambuliaji huyo anayefahamika kwa jina lingine kama El Pipita anasifika kwa kua na jicho la goli na kujua kufunga kwa kiwango kikubwa huku akipita vilabu vingi na kuonesha ubora wake wa kufumania nyavu.

Gonzalo Higuain amepita ndani ya Real Madrid ambapo amefunga takribani mabao 109 kwenye michezo 190 ya ligihuku akifanikiwa kubeba taji la La Liga mara tatu kabla ya kutimkia klabu ya Napoli mwaka 2013 pia huko alfanikiwa kucheza kwa kiwango bora huku akifanikiwa kuisaidia timu hiyo kubeba taji Coppa Italia huku akiwa na msimu bora kabisda mwaka 2015/16 baada ya kufunga mabao 36.

Mwaka 2016 wababe wa soka nchini humo klabu ya Juventus ilivunja rekodi kwa usajili wa ndani baada ya kumsajili mchezaji huyo kutoka Napolli kwa €90 milioni na kumsajili mchezaji huyo ambaye aliitumikia timu hiyo kwa misimu kadhaa na kufanikiwa kubeba mataji mawili ya Serie A huku akifanikiwa kufika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2017 kabla ya kutolewa kwa mkopo Ac Milan mwaka 2018 na baadae Chelsea ya nchini Uingereza na kufanikiwa kushinda michuano ya Europe League mwaka 2019 na baadae kurejea Juventus.

Gonzalo Higuain baada ya kumaliza mkopo wake klabu ya Chelsea alirejea Juventus ambapo aliondoka na kwenda ligi ya Marekani maarufu kama Major League Soccer (MLS) na kujiunga na klabu ya Inter Miami ambayo ameitumikia kwa misimu takribani miwili kabla ya kutangaza kustahafu hapo jana.

gonzalo higuainKwenye upande wa timu ya taifa pia mchezaji huyo ameitumikia timu ya Taifa ya Argentina ambapo alianza kuitumikia rasmi mwaka 2009 na kufanikiwa kuiwakilisha timu hiyo kwenye kombe la dunia mara tatu na Copa America mara tatu huku mafanikio makubwa yakiwa ni kuiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya pili mwaka 2014, Higuain ameitumiki Argentina michezo 75 na kufunga mabao 31 huku akiwa miongoni mwa wafungaji bora wa muda wote kwenye taifa hilo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa