Kiungo wa Leicester City Youri Tielemans ameshukuru kwa muhula wa mapumziko ya Kimataifa ambayo yametolewa kutokana na mwanzo mgumu akiwa na klabu hiyo, ingawa hajutii kusalia katika klabu hiyo.

 

Tielemans Hajutii Kusalia Leicester City

Leicester wamefanikiwa kutwaa pointi moja tuu katika mechi saba walizocheza na kupoteza kila mechi kati ya  sita walizocheza. Miongoni mwa vipigo hivyo ni 5-2 kutoka kwa Brighton, 6-2 kutoka kwa Spurs, huku matokeo hayo ya Jumamosi yakiongeza joto kwa Brendan Rodgers.

Tielemans alihusishwa sana na kutaka kuondoka Leicester wakati wa dirisha hili la usajili la hivi  majuzi zaidi, huku wakikabiliwa na uwezekano wa kupoteza thamani ya mkataba wake utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Ingawa hakuna hatua iliyofikiwa, Tielemans hajutii kubaki King Power Stadium, lakini kiungo huyo ambaye ndiye mfungaji wa bao la ushindi la Leicester dhidi ya Chelsea kwenye fainali ya kombe la FA 2020/21, amefarijika kuondoka kwenye hali mbaya na kujiunga na timu ya Ubelgiji.

 

Tielemans Hajutii Kusalia Leicester City

“Ninafuraha kupata hewa safi hapa katika majukumu ya Kimataifa kwasababu ni ngumu kwa Leicester hivi sasa” alisema katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi za ligi ya Mataifa ya Ubelgiji dhidi ya Wales na Uholanzi.

“Ni wazi kuwa mambo hayaendi vizuri katika klabu, tunafanya kila liwezalo kama timu. “Pale Leicester kushindwa mfululizo kumeathiri kama kundi. Tunahitaji kufaidika na mapumziko haya ili kuchaji betri hizi”.

Tielemans anasema kuwa ni vigumu kuliondoa hilo akilini mwake kwani linapita kichwani kwake,  na ni watoto peke yake wanaofanya asilifikirie suala hili.

Arsenal ilikuwa ni miongoni mwa vilabu vilivyohusishwa pakubwa na kumsajili mchezaji huyo wakati wa dirisha hilo la usajili, na anaahidi kuvutia vilabu vingi mwezi Januari ikiwa hatasaini mkataba mpya kabla. Lakini kiungo huyo anahisi fomu ya Leicester na hali yake ya kimkataba ni mada tofauti kabisa.

 

Tielemans Hajutii Kusalia Leicester City

Alisema hatazungumza sana kuhusu mkataba wake kwasasa na mambo yanazidi kuwa mabaya klabuni hapo ambapo haimfanyi yeye ajute kusalia klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa