BILIONEA Kijana na Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Dewji amemmwagia sifa, mlinda mlango namba moja wa timu hiyo Aishi Manula baada ya ushindi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika siku ya Jumapili 18 Septemba, 2022.

 

MO Dewji Amsifia Manula.

Klabu ya Simba SC walifanikiwa kufuzu hatua ya kwanza, kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini Malawi.

 

MO Dewji Amsifia Manula.

MO Dewji aliposti kipande cha video kilichoonesha magoli mawili ya Klabu hiyo waliyofunga kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, na kuandika maneno ya kumsifia kipa wa Simba SC.

“Ninakiri kwamba Aishi Manula ni miongoni mwa walinda mlango bora zaidi kwa sasa barani Afrika”

Manula amekuwa na kiwango kizuri kwa misimu takribani 3 sasa, akiwa na klabu hiyo kulingana na nafasi yake ya kuwa mlinda mlango namba moja kwenye klabu hiyo na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa