TAJIRI Kijana na Mwekezaji wa klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji amempongeza mwanamichezo nguli wa Tenisi Roger Federer baada ya kutangaza kustaafu mchezo huo.
MO Dewji ameungana na wadau na mashabiki wengine duniani kumtakia nyota huyo mwenye mafanikio makubwa kwenye tenisi akiwa ameshinda fainali 20 za Grand Slams na ushindi mara 8 wa Wimbledon katika tasnia yake.

MO Dewji Ampongeza Roger Federer

Kupitia akaunti ya tajiri huyo kijana barani Afrika aliandika ujumbe wake kwenda kwa Roger:

“Pongezi kwa Roger Federer katika taaluma yake nzuri ya tenisi, fainali 20 za Grand Slams na 8 ya Wimbledon, ambayo ameshinda zaidi kuliko mwingine. Moja ya wanamichezo wakubwa wa tenisi utakayekumbukwa”. Alisema MO Dewji.

MO Dewji Ampongeza Roger Federer

Wiki iliyopita nyota huyo alitangaza kustaafu mchezo huo ambapo ataenda kujiunga na mwanamichezo mwenzake Serena William ambaye naye amestaafu mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa