WAKIJIANDAA na mchezo wao wa Ligi dhidi ya Tanzania Prisons, benchi la ufundi la Ihefu limefunguka kuwa wanahitaji kuanza ligi na Tanzania Prisons.

Tangu wapande ligi kuu kwa msimu huu, kikosi cha Ihefu hakijafanikiwa kupata ushindi wowote wakiwa wamecheza mechi nne za ligi.

Ihefu wanatarajia kucheza mchezo wao wa tano kesho jumanne dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali, Mbeya.

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Msaidizi wa Ihefu, Temmy Felix amesema kuwa: “Maandalizi kwa upande wetu yamekamilika mpaka sasa na tutawakosa wachezaji watatu kwenye kikosi ambapo wawili ni wagonjwa na mmoja yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa.

“Tunawaheshimu Tanzania Prisons wana wachezaji wazuri na benchi lao la ufundi ni zuri lakini sisi kwa upande wetu tunahitaji pointi tatu ambazo ni muhimu sana katika kujitoa kwenye nafasi tuliyopo.

“Ninawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani hapo kesho ili kuwapa sapoti wachezaji wetu watakapokuwa kwenye kibarua cha kusaka ushindi wa kwanza kwa msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa