Scouting network ya Sir Alex Ferguson ilikuwa kali sana, watu wake walikuwa na uwezo wa kuona vipaji hata kama vimejificha nyuma ya Milima ya Alps huko Italia, au Sofia huko Bulgaria hata Fujiyama nchini Japan au Busan huko Korea Kusini
Miaka yote Sir Alex alikuwa anacheza sana soka la counterattack na kulinda shape zaidi, alikuwa haihitaji tu wachezaji bali wachezaji ambao ni Mashine na wanaweza kwenda kufanya kile anachotaka kwa asilimia 100
Ilikuwa jioni moja ya 1998, wakati huo Class of 92 kutoka Carrington imeanza kufanya maajabu makubwa kwenye soka la England, Kiungo cha United kilikuwa na mtu kama Nick Butt, Roy Keane na Paul Scholes, kazi ya mikono ya Marehemu Eric Harrison.

Jioni ile 1998 Fergie alisikia kuhusu kipaji cha kijana wa Scotland anaitwa Darren Fletcher, hapo ana miaka 15 tu ndipo akafuatilia Mawasiliano yake na kupiga simu nyumbani kwake usiku wa saa 2:15, simu ilipokelewa na Dada yake Fletcher, kisha akampasia Fletcher mwenyewe.

Ghafla kabla Fletcher hajashika simu akatokea Mama yake na kuipora simu kisha kumfokea sana Sir Alex kuwa anapiga vipi simu kwa Mtoto bila mzazi kuwa na taarifa kisha akamkatia simu, Fletcher alilia sana, Mama yake akagundua baadae aliemfokea ni Fergie ambaye ni Kocha wa Manchester United.
Walidhani labda ni stori za Mbuzi wa masikini hazai ila ghafla wakaona tena simu inaita, Sir Alex alipiga kwa mara ya pili akaomba radhi kisha akaomba ruhsa ya kuonana na Darren Fletcher kesho yake pale Carrington, huyu ndie Sir Alex bwana, muulize Mama yake Cristiano Ronaldo anamjua vyema

Kesho yake wakati Fletcher anaripoti kujiunga na United, Magwiji wengi wakawa wanamshangaa huyu mtoto mwembamba hivi ndie akawe mrithi wa Roy Keane? Paul Scholes? Au Nick Butt? Lakini dunia haikumuelewa Sir Alex yeye alikuwa na namna yake juu ya mtoto yule
Baada ya miaka takribani 10 mbele utakubaliana na mimi kuwa United walichapwa 2-0 Fainali ya UEFA pale Roma na Barcelona 2009, kutokana na kukosekana kwa Fletcher pia, hii ilikuwa Injini, Mourinho akiwa kama Mchambuzi alisema kabla ya mchezo Iniesta na Xavi wataenjoy leo bila Fletcher

Huyo ndio Sir Alex na Darren Fletcher wake “The Teacher’s Pet”
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.



Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
Fatina mfingi
Nice
Venerose
Safi sana
Adelta
Inapendeza Sana
neema hassan
Nice
Sarah
Safi sana
Caroline
Uyo ndo fagaaa
Hopemwaikuka
My fav coach
warda
United wakiyumba tu wanamkumbuka ferguson