Lautaro Martinez yuko tayari kusaini kandarasi mpya huko Inter, na anasema kwenda Barcelona ilikuwa ni zamani.

Lautaro: Kwenda Barcelona Ilikuwa ni Zamani

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 23, alikuwa na hamu kubwa kutimkia Barca mwaka jana wakati klabu ilipojiandaa kuondoka kwa Luis Suarez.

Suarez aliondoka kwenda Atletico Madrid wakati Barca, iliyokuwa na shida za kifedha, ilibaki na Lionel Messi, Antoine Griezmann na Martin Braithwaite kama chaguzi kuu kuu kwenye ushambuliaji.

“Ni kweli, nilikuwa kwenye mazungumzo na Barcelona,” Martinez aliiambia Gazzetta dello Sport.

“Nilikuwa wazi na Antonio Conte, nilimwambia: ‘Ninafikiria tu juu ya Inter, hii haitaniathiri’.

“Lakini, yote ni ya zamani. Nitaenda kusaini nyongeza ya mkataba na Inter.

Tangu ajiunge na Klabu ya Mashindano mwaka 2018, Martinez ameibuka kama mmoja wa washambuliaji chipukizi zaidi kwenye mchezo huo.

Alivutia msimu uliopita na mabao 21 katika michezo 49 lakini anaonekana kuzidi idadi hiyo msimu huu 2020-21, akiwa tayari amezitikisa nyavu mara 15 katika mechi 33.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

Lautaro, Lautaro: Kwenda Barcelona Ilikuwa ni Zamani, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa