Sir Alex Ferguson na Safu Nzuri ya Ulinzi Itakushindia Mataji

Sir Alex Ferguson aliwahi kusema, “Safu nzuri ya ushambuliaji itakushindia mechi lakini safu nzuri ya ulinzi itakushindia mataji” Fergie alikuwa sahihi ujue. Jana Chelsea wangekuwa makini kwenye ulinzi Pengine wangeshinda tatu kwa moja. Wameruhusu mabao mawili kwa makosa binafsi. Kosa binafsi la Marcos Alonso na Thiago Silva.

Hivi mmewaona Chelsea wanavyokaba? Bado sijaielewa ile ‘pressing’ yao. Pasi moja tu inawaacha washambuliaji wote. Pasi nyingine moja inawaacha viungo wote. Bado sijawaelewa! Tunaweza kuwa tunawalaumu mabeki, ila ‘Chemistry’ nzima ya ukabaji wa Chelsea ina matatizo. Kwa hili nipo tayari kukosolewa. Chelsea wana tatizo la kukaba kama timu. Sijui ni hawajamuelewa mwalimu au plan ya mwalimu ndio mbovu.

Marcos Alonso si mzuri wa kupora mipira, si mzuri kwenye ‘one on one’ situation akiwa na mpinzani na si mzuri wa kufanya interceptions. Anawapa mzigo mkubwa sana mabeki wa katikati wanaposhambuliwa. Marcos Alonso unampenda tu wakati anashambulia. Unapotumia mfumo wa mabeki wanne, Alonso hakupi kila unachohitaji kutoka kwa ‘full back’. Ana-fit zaidi kucheza wing back. Kama Lampard anafikiria kuendelea kucheza na ‘four man defender’ nadhani ni muda wa kukubali ile ofa kutoka Inter ya kumuuza Alonso. Chillwell akiwa fit atampa zaidi anachohitaji.

Yule Timo Werner ni mtu sana. Anapokuwa na mpira, anafikiri kitu kimoja tu, kushambulia. Positioning yake ni ya viwango sana. Muda wa kuwa pembeni anakuwa pembeni, muda wa kuwa katikati anakuwa katikati, muda wa kukimbia anakimbia na muda wa kutembea anatembea. Jana amechezeshwa pembeni kisha akachezeshwa mshambuliaji wa pili alipoingia Giroud, na bado alikuwa hatari. Siku Lampard atakapomchagulia jukumu mama. Atatisha zaidi.

Mason Mount ni tunda la uaminifu wa kocha kwake. Amezidi kujiamini, anaielewa mikimbio ya wenzake wanapofika kwenye tatu ya mwisho ya uwanja. Amekuwa mapema sana. Kai Haveirtz anazidi kuzoea. Callum Hudson-Odoi amempa swali gumu sana Lampard jana. Hajajalisha Uwepo wa jina la Ziyech na Pulisic. Amepewa nafasi na ameitumia vema. Kama ataendelea hivi waatakaporejea akina Pulisic, ipo siku Lampard atashindwa kupanga kikosi.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

36 Komentara

    Ukimzungumzia fergie ni kocha ambaye alikuwa na falsafa ya kipekee katika mpira

    Jibu

    Alikuwa na team nzuri

    Jibu

    Alex alikua kocha hodari na mwenye kipaji cha ukocha pongezi sana ferguson kwa kazi nzuri

    Jibu

    alex alikuwa kocha makini mwenye umahili mzuri katika kufundisha

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Me naona wachezaji wa Chelsea bado hawajamuelewa kocha

    Jibu

    Nikweli kabisa Ferguson nibonge lakocha lakistoria alikuwa anajua nini anafanya ndomana amestafu nakipaji chake namkubali Sana Mzee huyo alikuwa anatikisa Sana babu Farguson

    Jibu

    Ferguson yupo sahihi kabisa na kila klabu aliyokuwa akiiongoza lazima wachezaji wawe fiti uwanjani na wanafanya vizuri sana

    Jibu

    Habari njema sana

    Jibu

    Alex alikua ni kocha mzuri sana katika kufundisha kikosi

    Jibu

    Vzr sana

    Jibu

    Habari safii sana

    Jibu

    Achan na uyo mwamb Ni hatar sanaa

    Jibu

    Ni mtazamo wake

    Jibu

    Chelsea wazzur sema safu ya ulinz bado ina mapungufu

    Jibu

    Kocha yuko vizuri

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    Nmeilewa hii

    Jibu

    Safi yupo vizuri

    Jibu

    Sir Alex ferguson ni mmoja ya makocha Bora ulimwenguni na maneno yake yanaishi mpka leo kwny mchezo wa mpira wa miguu ni kwl kabisa gud defence mataji uhakika na ukiwaha na washambuliah wazuri utapata magoli tu hutowez kwn huku kwn watakufah wanafungah na ww unafungah ila ukiwez kuwah nawalinzi imara wawez kusogeah mbele kufunga na kulinda goli

    Jibu

    alex alikuwa kocha makini

    Jibu

    saf

    Jibu

    Tangu aondoke man u haijawahi kupata tena kocha mzuri kama huyu

    Jibu

    Ni kwer ni mbin inayofany opponent wako asije gorin kwako

    Jibu

    Saf

    Jibu

    Safu ya ulinzi ikiwa imara ndio utakapopata ushindi kwenye mechi ni bora fowad wakawa butu ila mabek imara

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Sr Alex Ferguson ni kocha mankini sn

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Hatari sanaa

    Jibu

    alikua sahihi

    Jibu

    hawakukosea kumpa cheo cha Sir Alex Fergason

    Jibu

    Sir Alex ferguson ni mmoja ya makocha Bora ulimwenguni na maneno yake yanaishi mpka leo kwny mchezo wa mpira wa miguu ni kwl kabisa gud defence mataji uhakika na ukiwaha na washambuliah wazuri utapata magoli tu hutowez kwn huku kwn watakufah wanafungah na ww unafungah ila ukiwez kuwah nawalinzi imara wawez kusogeah mbele kufunga na kulinda goli

    Jibu

Acha ujumbe