Mchezo wa soka ni kati ya vitu ambavyo uwezo wa mchezaji haufichiki kwa namna yoyote ile ikiwa na maana kwamba uhalisia wake upo wazi sana na hakuna kitu kinaweza kufanyika bila kuonekana na kukubalika machoni mwa wengi. Hivyo, sio rahisi kabisa nyota mmoja kukubalika na mtu mmoja mmoja bali huwa ni jambo lisilofichika kabisa.
Wafuatao ni baadhi ya nyota ambao kwa hakika wataanza kunyemelewa kwa kasi sana na klabu kubwa nyingi barani Ulaya wakiwa katika umri wao mdogo wa miaka 21 na wengine wakiwa hata bado hawajaufikia umri huo. Baadhi ya nyota hao ambao wataweza kusumbua vichwa vya wakubwa wengi ni kama vile:
Luka Jovic, ni ndani ya muda mfupi tu klabu ya Eintracht Frankfurt imempa mkataba mzito nyota huyo ikiwa wao wameumnunua kwa kiwango cha chini kabisa. Kwao itakuwa biashara ya aina yake kwa sababu kwa hakika hawawezi kuumiza vichwa sana kutokana na faida ambayo wataitengeneza. Tayari baadhi ya klabu zenye majina makubwa zimeanza kumuwinda nyota huyo raia wa Serbia wakiwemo Barcelona, Bayern Munich, Chelsea na Real Madrid.
Matthijs de Ligt, Ajax ndani ya kikosi chao wamekuwa na nyota wengi sana ambao kwa hakika watakuja kuwa tishio kutokana na uwezo wao na viwango vyao vya pekee. Vijana hao wameisaidia klabu hiyo kuvuka hatua zote za klabu bingwa nusu fainali na hadi kufika hapo mchango wa nyota huyo ulikuwa mkubwa sana na wa pekee.
Jadon Sancho, kwa hakika jina la nyota huyu limeshika nafasi katika maeneo mengi ya Ujerumani kutokana na uwezo wake wa pekee kwa umri wake mdogo. Hili ni zao tumainiwa la taifa la Uingereza, atakuwa nyota wa kutumainiwa sana. Tangu ahamie Ujerumani kujiunga na Dortmund amewavutia vigogo wengi kuhitaji huduma yake wakiwemo Manchester United.
Joao Felix, miongoni mwa nyota waliotokea katika kikosi cha kukuzia soka cha Benfica ikiwa ni sehemu ya kundi la nyota wengine waliolelewa humo kama Bernardo Silva, Ederson Moraes na Joao Cancelo. Kwa hakika amedhihirisha ubora wake akiwa na kikosi hicho cha Benfica baada ya kupandishwa kuanza kuhudumu kwenye kikosi cha wakubwa. Anaonekana kuwa na uwezo wa pekee hapo baadaye, ni mbegu ya kuikuza zaidi.
Kai Havertz, Bayern Leverkusen wana majina mengi ambayo uwezo wao ni wa kipekee sana na wanaweza sana kuiletea mapato na upekee wa aina yake klabu. Baadhi yake ni watu kama Leon Bailey na Julian Brandt ambao wanajua kazi yao wakiwa uwanjani. Ni kizazi cha kutegemewa katika soka iwe kama watasalia ndani ya klabu zao hizo au watazihama. Uwezo wa Havertz umekuwa juu sana na majirani Bayern Munich wameshaanza kubisha hodi kumhitaji.


Povel
Gud news