Stori za EL Classico: Real Madrid 2-0 Barcelona

Stori za El Classico! Kinachobamba kwenye mechi Real Madrid na Barcelona wanapokutana.
_
Yule mtoto,Yule mbrazil, yule Vinicius Junior anastahili kuwa namba moja hapa kabisa. Msimu wa pili akicheza Madrid amekuwa na nyakati mbaya na nzuri. Ameishi maisha ya uvulana wa Walcott. Mara nyingi atajichukulia mtaa wa wapinzani awaache hawajui nini cha kufanya ila unajua tu hatakuwa na mwisho mzuri, atapiga pasi ya mwisho mbovu au apaize juu. Ila leo haikuwa hivo, kila alipokuwa na mpira alikuwa kitanzi kwa back line ya Barca, zaidi leo alijua lilipo goli. Ni uzuri tu wa Miguu ya Terstegen ilimnyima brace.
_
Setien? Kwanini lakini mzee wangu? Kwanini 4-4-2. Au kwasababu Pep alishinda nayo katikati ya wiki. Umesahau Huna wachezaji kama wa pep. Tofauti na La Pulga nani mwingine ana mbio kama Mahrez, De Bruyne na Gabriel Jesus. Huna kabisa hao watu mzee wangu. Kwanini usingekuja na mfumo wako wa kila siku. Umewaangusha vijana wako. Hata kama wanafungwaga Santiago Bernabeu hawapigiwagi mpira vile. Ungewafurahisha hata kwa kabumbu safi kama ushindi hauwezekani. Umewaangusha Barca mzee wangu.
_
Tuseme nini juu ya Fede Valverde. Kuna mtu ana wasiwasi naye tena? Mtu fulani mwenye miguu ya chuma akiwa anakimbiza mpira, mtu fulani mwenye miguu mlenda akipiga pasi, kiungo halisi wa Kiuruguay. Maamuzi sahihi ya eneo la kuwepo kucheza mpira, maamuzi sahihi ya eneo la kupeleka mpira. Mtu flani mjanaja sana kwa kufanya pressing. Aliwaweka jela viungo wa Barca.
_
Dani Carvajal, hata kama hakuwa man of the match huwezi kuiacha miguu ya yule mwanaume. Aliongeza idadi ya viungo alipovuka mstari wa kati, aliongeza idadi ya washambuliaji alipofika kwenye tatu ya mwisho, alikuwa beki kisiki waliposhambuliwa. What a player.
_
Hata kama Barca wamefunga huwezi kumuacha Semedo. Licha ya kuwa kwenye gereza la Vinicius bado alikuwa bora sana. Timing zake wake wakati wa kukaba, ubora wake kupandisha timu. Brilliant boy. Cancello ana kazi kupata namba timu ya taifa pale Ureno.
_
Siwezi thubutu kumaliza bila kuitaja mikono ya wale Binadamu wawili kwenye vijiti. Stegen na Courtois, watu sana. Saves kadhaa maridadi sana. Wanazidi kuwapa kazi watakaotoa tuzo ya Golden gloves.

3 Komentara

    Wakikutana lazima wafungane hiyo Ndio history yao

    Jibu

    Kanajua sana.

    Jibu

    Madrid wapo vizur sana

    Jibu

Acha ujumbe