WAKITARAJIA kumenyana na Simba leo straika wa Azam FC, Abdul Sopu amerejeshwa kikosini baada ya kugundulika kutokuwa na majeraha yeyote.

Sopu ambaye alijiunga na Azam msimu huu akitokea Coastal Union alikuwa nje ya kikosi akisubiri ripoti za madaktari wa timu ili aweze kurejea uwanjani.

Mchezo huo wa ligi kuu kati ya Azam dhidi ya Simba unatarajiwa kupigwa leo alhamis saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa.

Akizungumzia hilo, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema “Simba ni timu kubwa na nzuri zaidi ukizingatia rekodi walizonazo.

“Kikubwa kwa mashabiki wa Azam FC ni kurejea kwa kiungo wao Sospeter Bajana ambaye alikuwa kwenye mapumziko mafupi ya kifamilia.

“Pia ripoti ya madaktari ambayo imeeleza kuwa mshambuliaji Abdul Sopu hana majeraha yeyote ambayo yatamuweka nje hivyo ikimpendeza kocha Kali Ongala atamtumia kwenye mchezo wa leo.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa