NYOTA wa kikosi cha Geita Gold, Saido Ntibazonkiza amefunguka kuwa kila mchezo kwake ni fainali kwa ajili ya kuhakikisha timu yao inakuwa katika nafasi nzuri.

Saido kwenye mchezo wa jana jumatano dhidi ya Ruvu Shooting amefanikiwa kutoa assist ya bao lililofungwa na Juma Mahadhi huku yeye akifunga bao la ushindi ambapo mchezo huo ulimalizika kwa mabao 2-1.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Saido alisema “Namshukuru Mungu mchezo umemalizika salama na tumepata ushindi katika mchezo wa leo.

“Mchezo ujao tutacheza na Yanga hivyo tutaenda kujiandaa ili kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo tukishirikiana.

“Mimi kama mchezaji mzoefu kwenye timu kila mchezo kwangu ni fainali na hii ni katika kuhakikisha kuwa tunapata pointi tatu katika kila mechi na timu inakuwa kwenye nafasi nzuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa