Takribani watu 129 wamefariki huku wengine 180 wakijeruhiwa baada ya ghasia kuzuka kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Indonesia ya Liga 1 kati ya wapinzani Arema Malang na Persebaya Surabaya siku ya Jumamosi.

 

Takribani Watu 129 Kwenye Ligi Kuu ya Indonesia

Kufuatia vurugu hizo polisi walirusha mabomu ya machozi katika jaribio la kuwatawanya mashabiki hao waliokuwa wakileta ghasia na kukanyagana uwanjani baada ya wenyeji Arema kupoteza mchezo kwa mabao 3-2.

Mkuu wa polisi wa Java Mashariki Nico Afinta alisema watu walikufa baada ya kukandamizwa na kukosa hewa walipokuwa wakigombea njia hiyo hiyo ya kutoka. Afinta alisema watazamaji 3,000 kati ya takriban 40,000 waliohudhuria walivamia uwanja na kuanzisha “machafuko”, na kulazimisha usalama na polisi kuingilia kati na mabomu ya machozi.

Takribani Watu 129 Kwenye Ligi Kuu ya Indonesia

Picha zilizonaswa kutoka ndani ya uwanja huo zinaonyesha watu wakiruka juu ya uzio, huku nje ya uwanja huo kukiwa na magari yaliyoteketezwa, likiwemo gari la polisi. Huku mkuu wa afya wa eneo hilo Malang Widjanto Widjoyo akisema kuwa idadi ya watu waliofariki ni takribani 129.

Chama cha Soka cha Indonesia (PSSI) kimetangaza uchunguzi kuhusu chanzo cha fujo huo na tayari kimemfungia Arema kuandaa michezo kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu.

Takribani Watu 129 Kwenye Ligi Kuu ya Indonesia

“Tunajutia hatua ya wafuasi wa Arema katika Uwanja wa Kanjuruhan,” mwenyekiti wa PSSI Mochamad Iriawan alisema. “Tunatoa rambirambi na kuomba radhi kwa familia za wahasiriwa na wahusika wote kwa tukio hilo.”

Chama cha soka nchini hapo pia, kimesimamisha mechi za wikiendi zote za Liga 1 kufuatia idadi ya watu hao kufariki kwa takribani 129. Indonesia imeratibiwa kuandaa Kombe la Dunia la Vijana wasiozidi umri wa miaka 20 2023 mwezi Mei na Juni.

Waziri wa Michezo na Vijana Zainudin Amali alisema kuwa wanasikitishwa na tukio hilo ambalo linaumiza, soka letu wakati ambapo mashabiki wanaweza kutazama mechi. Pia alisema kuwa atachunguza na kuangalia kama mashabiki waruhusiwe kuingia uwanjani au laah.

Takribani Watu 129 Kwenye Ligi Kuu ya Indonesia

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa