Jiwe walilolikataa waashi kule Stamford Bridge, linang’ara Turin. Tammy Abraham amekuwa mwiba ndani ya AS Roma msimu huu.
Baada ya kuonekana hana nafasi kwenye kikosi cha Chelsea, Tammy alijiunga na Roma mwishoni mwa msimu wa 2020/21. Akiwa chini ya Jose Mourinho, Abraham huyu sio yule wa Lampard kipindi kile.
Roma wamemaliza rasmi msimu wa 2021/22 kunako Serie A jana usiku ambapo, pamoja na kujihakikishia kucheza Europa msimu ujao, Abraham ameweka rekodi msimu huu.
Tammy Abraham amekuwa mchezaji wa kwanza (raia wa Uingereza) kupachika magoli mengi (17) kwenye msimu mmoja wa Serie A. Hii ni baada ya mshambuliaji huyu kupachika magoli 2 kati ya 3 waliyopata dhidi ya Torino.
Japokuwa bado anamkataba na Roma mpaka 2026, kuna mazingira ya sintofahamu kuhusu uwepo wa Abraham kikosini hapo msimu ujao. Uwezo aliouonesha msimu huu ni dhahiri, kuna vilabu vinamtolea macho kwa ukaribu na, huenda lolote likatokea kwenye usajili wa majira ya kiangazi.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.