Fainali ya Western Conference kunako NBA inaendelea kunoga kati ya Golden State Warriors na Dallas Mavericks. Vijana wa Kerr wanajambo lao msimu huu.

Baada ya kuwa na msimu mbaya mwaka jana, Warriors wamerejea kwa kishindo msimu huu. Steph Curry ameendelea alipoishia, ni mwendo wa kutupia vikapu kwa kila namna.

Mchezo wa 2 kati ya Warriors na Maverick umemalizika kule California ambapo, licha ya Mavericks kuongoza kwenye ungwe ya kwanza, Curry na wenzake walipindua meza kwenye ungwe ya pili na kujiweka kwenye njia ya ushindi.

Kutoka kuongozwa kwa pointi 19 mpaka kumaliza mchezo kwa ushindi wa pointi 126-117 na, hii inawapa fursa Golden kuongoza kwa matokeo ya 2-0 kuelekea kwenye mchezo wa 3.

Mavericks nao wanajulikana kwa kupindua meza. Walifanya hivyo kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Phoenix Suns ambapo, Suns waliongoza kwa michezo 2 ya mwanzo kabla ya Mavericks kupindua matokeo na kutinga fainali ya Western Conference.

Steph Curry alipachika jumla ya pointi 32 huku kinara akiwa ni Luka Doncic aliyepachika pointi 42 kwa Mavericks.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa