Erik ten Hag alitania kuwa huenda akahitaji kutafuta fedha kutoka kwa mashabiki wachanga wa Manchester United alipoulizwa kama klabu itawasajili Jude Bellingham na Kylian Mbappe.
United wanatarajiwa kuimarisha safu yao wakati wa usajili wa Januari, huku wakiendelea kuimarisha uamsho wao chini ya kocha huyo Mholanzi Ten Hag.
Uhamisho wa kiungo wa Borussia Dortmund Bellingham na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Mbappe, hata hivyo, hauwezekani kuwepo mezani.
Hilo halijawazuia mashabiki kumhoji Ten Hag kuhusu dili la mchezaji yeyote, ambapo Teh Hag alitania kwamba huenda akahitaji zaidi ya kuungwa mkono na bodi ili kutafuta uhamisho wowote.
Aliliambia kundi la mashabiki wachanga ambao walimuuliza kama angeweza kununua jozi hizo., na akasema “Je! una senti kwa ajili yangu?”
United haitakuwa na haja ya kuzama kwenye mifuko ya mashabiki wao ili kutimiza hatua zozote dirisha hili, ingawa ni nani Ten Hag atamleta kupitia mlangoni bado haijajulikana.
Jack Butland ameletwa kwa mkopo kutoka Crystal Palace kuchukua nafasi ya Martin Dubravka, ambaye amerejea Newcastle United, huku United pia wakitajwa kumtaka Wout Weghorst, mshambuliaji ambaye yuko kwa mkopo Besiktas kutoka Burnley.
Kiungo wa kati wa Uingereza, Bellingham anapendekezwa sana kuondoka Dortmund baadaye mwaka huu, huku Liverpool, Real Madrid, Chelsea na Manchester City zote zikitajwa kumtaka.
Mshambuliaji wa Ufaransa Mbappe aliongeza muda wake wa kusalia PSG mwezi Mei mwaka jana.