Mchakato wa kumsaka kocha mpya wa Manchester United unaendelea kushika kasi. 1 kati ya 4 wanaotajwa, ameanza mazungumzo. Erik Ten Hag ahojiwa.
Ni kawaida kabla ya kupata kazi, huwa kuna mahojiano ya awali kati ya muajiri na anayetarajia kuajiriwa. Manchester United ni hivyo hivyo, Ten Hag amefanyiwa mahojiano ya awali kule Old Trafford.
Mholanzi huyu ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa Ajax, amekuwa akihusishwa na Man United toka Ole Gunnar Solskjaer alipoondolewa klabuni hapo. Japokuwa Erik hana uzoefu na EPL, lakini amepata mafanikio makubwa akiwa na Ajax toka mwaka 2018.
Awali kulikua na mashaka ya uwezo wake wa kuzungumza lugha ya kiingereza lakini, Erik anaonekana kuwa na uwezo mzuri wa kuzungumza lugha hiyo na hivyo, kipengele cha mawasiliano kwake hakitakua changamoto kama ilivyodhaniwa na wengi.
Inasemekana, katika majadiliano hayo, Ten Hag aliiuliza bodi ya United kuhusu mpango wa muda mrefu wa klabu hiyo pamoja na bajeti wanayopanga kuitumia katika mabadiliko makubwa ya klabu hiyo.
Ikumbukwe kuwa, mchakato wa kocha mpya wa United haumtegemei Erik peke yake. Mauricio Pochettino, Julen Lopetegui na Luis Enrique ni miongoni mwa makocha wanaotarajia kufanya mazungumzo na bodi ya Man United.
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.