Tujikumbushe Kuhusu Mechi Ndefu Zaidi ya Soka!

Tujikumbushe!

Mechi ya kawaida ya soka inatakiwa kuisha ndani ya dakika 90. Unaweza kufikiria gemu ikizidi zaidi ya hapo inaweza kuwa na mda gani?

Siku hizi gemu za kawaida, soka la kulipwa linachezwa dakika 90 na pia kwa mazingira fulani mechi inaweza kuongezeka mda, hasa kwenye michuano ya mtoano, gemu inaweza kwenda hadi dakika 120. Haitakiwi kuzidi mda huu kwa mujibu wa sheria za soka.

Hata hivyo, wajuzi wa mambo bado wamekuwa wakikosoa sana kuongeza vipindi viwili vya dakika 15 baada ya zile 90 kukamilisha 120 kwenye soka la kulipwa.

Kumekuwa na changamoto kadhaa katika soka la kitaalamu! Soka la kukusanya mpunga, au soka la kulipwa katika umaarufu wake. Wachezaji wamekuwa wakichoka na kupata majeraha mbali mbali, hivyo dakika 120 zenyewe zinaonekana ni changamoto, unaweza kumaliza karibu nusu ya kikosi wameshaumia kama sio kuchoka sana kiasi cha kuhitaji mda zaidi mpaka kuingia kucheza mechi inayofuata.

Sasa, unaweza kuamini kuwa kuna kipindi mechi zilichezwa kwa mda wa zaidi ya mda tuliouzoea? Wacha tujuzane hapa, kuamini inabaki kuwa jukumu lako na ukisakua sakua ukweli huku na kule!

Mechi ndefu zaidi kwenye soka iliyochezwa masaa 3

Mechi ndefu zaidi kuwahi kurekoidiwa kwenye soka, ilikuwa ni klabu za Stockport County dhidi Doncaster Rovers kutoka Uingereza, March 30, 1946. Mechi hii ilichukua jumla ya masaa 3 na dakika 23.

Gemu hii imeishi kwenye rekodi ya dunia, kama mechi ndefu zaidi ya soka kwa zaidi ya nusu karne. Kimsingu hii ilikuwa gemu ya pili ya League III North Cup, ya kwanza iliisha kwa sare ya 2-2. Na gemu ya pili pia ikaisha hivyo hivyo na kulazimika kuendelea kwa mda wa nyongeza. Waliendelea kucheza kwa mda bila kupatikana kwa goli lolote. Baadaye kidogo katika mda wa nyongeza mshambuliaji wa Stockport, Les Cocker alicheka na nyavu!

Mechi Ndefu Katika Historia ya Soka, Masaa 3!

Mashabiki wa Stockport waliruka kwa furaha na kelele nyingi kushangilia mpaka walipozimwa na kipyenga cha refarii bwana Baker aliesema kuwa alishuhudia mpira kushikwa na hivyo halikuwa goli. Gemu iliendelea na wachezaji walichoka sana, wakawa wanaanguka hovyo hovyo dimbani. Mshabiki walimlilia refa amalize mpira.

KIlichofanyika ni kutumia mbinu ya kurusha shilingi ili kumpata mwenyeji wa mechi itakayofuata ya marudiano hadi wahakikishe anapatikana mshindi. Doncaster walipata nafasi ya kuwa wenyeji, na kuwakaribisha washindani wao, mechi iliyofuata ya marudiano wenyeji Doncaster walishinda bao 4-0.

Baada ya hapo, sheria ya “Play to Win”, yaani kusakata kabumbu hadi pale anapopatikana mshindi ambayo ilishika hatamu kipindi hicho katika soka la Ulaya ilifika tamati mda mfupi baadaye.

 


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe