Ten Hag: Maguire Sio Chaguo la Tano

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema kua nahodha wa klabu hiyo Harry Maguire sio chaguo la tano ndani ya klabu hiyo kama ambavyo watu wanazungumza huko nje.

Harry Maguire ameonekana kukosa nafasi chini ya mwalimu Erik Ten Hag kwani beki huyo amefanikiwa kuanza kwenye michezo michache sana chini ya kocha huyo, Kutokana na suala hilo limepelekea watu wengi kufikiri beki huyo hana nafasi kwenye timu hiyo kwasasa.Ten HagHarry Maguire ameonekana kutumika kama chaguo la tano mara kadhaa hilo ni jambo ambalo limeonekana licha ya kocha huyo kukanusha, Kwani safu ya ulinzi ya timu hiyo ina mabeki wanne wa katikati Varane, Martinez,Lindelof, na Maguire, Lakini kocha huyo alifikia hatua ya kumpanga beki wa kushoto Luke Shaw kama beki wa katikati kipindi ambacho Maguire yupo kwenye benchi.

Kocha Erik Ten Hag anasema beki huyo si chaguo la kwanza na anatakiw kupambana ili aweze kuirejesha nafasi yake ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, Na kocha huyo amesisitiza kua vitu hua vinabadilika haraka sana hivo mchezaji huyo anaweza kupambana akairudisha nafasi yake kikosini haraka sana.Ten HagBeki Harry Maguire anapaswa kupambana ili kurejesha nafasi yake ndani ya kikosi cha Manchester United ambayo inaonekana imepotea, Nahodha huyo ambaye alifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Uingereza ameelezwa na kocha wa klabu hiyo anapaswa kupambana ili kurejesha nafasi yake kikosini.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.