Mchezaji wa tenesi raia wa Uswisi – Roger Federer amerejea tena uwanjani ikia ni miezi 14 tangu alipocheza mchezo wake wa mwisho.
Federer alikuwa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goli mara 2 na aliikosa michuano kadhaa kabla ya kurejea kwenye mashindano ya Qatar Open 2021.
Bingwa huyu wa Grand Slam mara 20, alikuwa uwanjani akichuana na Muingereza- Dan Evans katika mchezo uliochezwa jijini Doha, Qatar.
Roger Federer aliibuka kidedea kwenye mchezo huo kwa kumbwaga Dan Evans kwa matokeo ya seti 7-6 (10-8) 3-6 7-5 na sasa amefuzu hatua ta robo fainali.

“Ninajisikia vizuri kurudi uwanjani. Ni vizuri kuwepo hapa iwe nimeshinda au nimefungwa, ni burudani.
“Sijui kama maumivu yataisha kabisa. Unajisikia mchovu na unashindwa kujua kama ni misuli au la. Kitu cha muhimu ni nitakavyojisikia kesho, keshokutwa na kwa miezi 6 ijayo.” Alisema Federer.
Federer ambaye ni bingwa mara 3 wa mashindano ya Qatar Open, atachuana na Nikoloz Basilashvili kwenye mchezo wa robo fainali.
warda
Hata mie nimefurahia ujio wake
Venerose
Roger karibu tena jukwaani
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri
Hopemwaikuka
Guud
Caroline
Yupo vizuri
Neema juma
Yuko poa sana
Sarah
Yupo vizuri
Issa
Safi san