Nyota Lionel Messi na Christiano Ronaldo kwa mara ya kwanza hawatoona timu zao zikiendedelea na michuano ya Champions League hatua ya robo fainali.

Messi na Barcelona waliondolewa na PSG ashindano hayo ya Ulaya katika hatua ya 16 bora baada ya kwenda sare ya 1-1 kwa jumla ya magoli 5-2.
Ronaldo na Juventus walitolewa kwa jumla ya magoli 4-4 lakini FC Porto walikuwa na faida ya goli la ugenini.
Mara ya mwisho mastaa hao kuondolewa na kukiosa nane bora, Messi na Barcelona walitolewa na Chelsea katika hatua ya 16 bora.
Wakati huohuo Ronaldo alikuwa Manchester United walitolewa na AC Milan pia walitolewa katika hatua ya 16 bora.
Kwa ujumla Ronaldo ameshinda mataji ya Champions League mara tano wakati Messi ameshinda mara nne mara ya mwisho ilikuwa 2014-15.
Messi akiwa na umri wa miaka 33 na Ronaldo akiwa na miaka 36 huenda utawala wao unelekea ukingoni baada ya kutokuwa na makali kwa misimu ya hivi karibuni.
Mbappe ambaye timu yake ya PSG imewatoa Barcelona na yeye akihusika kufunga mabao manne alivunja ya rekodi ya Lionel ya kuwa mchezaji mdogo kufikisha mabao 25 katika Ligi ya Mabingwa na bado huenda akaendelea kuongeza.
Erling Haaland pia aliweka kambani bao nne katika hatua ya 16 bora dhidi ya Sevilla akiwa na umri wa miaka 20 na amekuwa mchezaji kinda zaida kufikisha mabao 20 ya Champions League.
Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.
Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.



Venerose
Poleni sana
Lydia Emmanuel Magoti
Duuh pole yao
Hopemwaikuka
Kumbee
Caroline
Pole sana
warda
Bora wametupwa wote angetupwa CR7 peke ake ningeumia sana
Neema juma
Polee yaoo
Issa
Ligi imekua ngum