Mchezaji nyota wa timu ya Brooklyn Nets – Kevin Durant [KD] ameripotiwa kuendelea kukaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi.
KD hajarejea uwanjani tangu alipocheza dhidi ya Golden State Warriors (Februari 13 2021), hii ni baada ya kuumia nyonga ya kushoto.
Mchezo wa Nets vs Boston Celtics leo usiku utakuwa ni mchezo wa 10 mfululizo kwa Kevin Durant kukosekana uwanjani.
Kocha wa Nets – Steve Nash amethibitisha KD atafanyiwa uchunguzi mwingine siku chache zijazo na mpaka sasa, haijajulikana ni lini mchezaji huyo atarejea tena uwanjani.

“[KD] hajacheza kwa mwezi mmoja. Haijalishi matokeo ya uchunguzi yatasemaje, bado tunahitaji muda ili kuhakikisha anaumaliza msimu huu akiwa imara zaidi.
“Kwa sasa anaendelea vizuri na tunaimani chanya na muelekeo alionao lakini tunapaswa kuchukua tahadhari kwa sababu ni mchezaji wa muhimu sana kwetu.” alisema Nash.
Durant hakusafiri kwenda Atalanta kwenye michezo ya NBA All Stars na badala yake alibaki Brooklyn chini ya uangalizi wa madaktari wake.
Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.
Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.



Venerose
Pole sana Kelvin utapona tu
Lydia Emmanuel Magoti
Duu pole yake
Hopemwaikuka
Sorry for you
Caroline
Pole Key
warda
pole yake
Neema juma
Pole yake kijana
Sarah
Pole yake
Angelina
Pole yake
Issa
Durant pole