Tetesi zinasema Manchester United, na Chelsea zinamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23 mwenye thamani ya juu.

Barcelona wanafuatilia kwa karibu upatikanaji wa beki wa nyuma wa Arsenal Shkodran Mustafi, 28, na mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, 27, huku wachezaji hao wa kimataifa wa Ujerumani wakiwa hawatakiwi na klabu zao.

Arsenal na Tottenham ni miongoni mwa klabu kadhaa zenye nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg Dominik Szoboszlai, 20, huku RB Leipzig, AC Milan na Atletico Madrid pia wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Manchester United, Manchester City na Chelsea wanashindana kumsaini kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Uswiss Denis Zakaria, 24, mwezi Januari.

Tetesi zinasema Tottenham bado wanamtaka mlinzi wa Inter Milan na Slovakia -Milan Skriniar, 25, licha ya mazungumzo kati ya klabu hizo kuvunjika msimu uliopita.

Tetesi zinasema mlindalango wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 24, anaweza bado kufanikiwa kuhamia katika klabu ya Primia Ligi msimu ujao baada ya Tottenham na Chelsea kuacha nia yao.

Arsenal bado hawajaweka dau la kiungo wa kati wa Norwich Emi Buendia, 23, huku Muargentina huyo akiwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuchaguliwa kusaini mkataba na the Gunners.

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira, ambaye kwa sasa ni meneja wa klabu ya Nice, anataka kumleta katika klabu hiyo mchezaji wa Arsenal na Ufaransa-mlinzi William Saliba, 19.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.
 

Tetesi zinasema Juventus wanajiandaa kuongeza mara dufu dau lao kwa ajili ya beki wa Chelsea Muitalia Emerson Palmeri, 26, na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34.

Barcelona wamechagua mlinzi wa Atletico Madrid na Brazil Felipe Augusto, 31, kama mchezaji wao mbadala wa kuchukua nafasi ya Gerard Pique, 33, mwenye majeraha huku msimu wa Uhispania ukiwa umemalizika.

Tetesi zinasema mlinzi wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 20, yuko tayari kurejea Barcelona baada ya kushindwa kucheza hata dakika moja wakati wa mkataba wake wa mkopo Benfica.

Mchezaji wa safu ya kati wa Barcelona Riqui Puig, 21, ataruhusiwa kuondoka kwa mkataba wakati wa dirisha la uhamisho la wachezaji la mwezi Januari na mchezaji huyo wa timu ya Uhispani ya vijana walio chini ya umri wa miaka 21 amepewa fursa ya kujiunga na Leeds United, RB Leipzig na Monaco.

 

Wilshere

Tetesi zinasema Rangers wanaonekana wako tayari kumkosa mchezaji asiye na wakala Muingereza Jack Wilshere, 28, huku wakitaka kiungo huyo wa kati arejee Arsenal.

Arsenal wanaweza kutumia pauni milioni 32 iwapo wanataka kuendelea kuwa na wachezaji watano ambao mkataba wao unakamilika msimu ujao ili kuimarisha kikosi hicho katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa