Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller amezivutia Newcastle United na Everton, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akikaribia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake na timu hiyo ya Bundesliga.

Barcelona wanafanyia kazi mpango wa kuchangisha €100m (£83.5m) kufadhili usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 21 msimu huu.

Tetesi zinasema, Brighton wamekataa ofa kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya mlinzi wa Uingereza Dan Burn, 29.

Kiungo wa kati wa Lyon, Bruno Guimaraes ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kuhamia Newcastle, ambayo imewasilisha ofa mezani kwa Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 24.

 

Southampton wanatayarisha dau la rekodi la klabu la £25m kumpa Armando Broja kwa mkataba wa kudumu baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Albania mwenye umri wa miaka 20 kujiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea kwa mkopo wa msimu mmoja mwanzoni mwa msimu.

Newcastle wameanza tena mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Uholanzi Mitchel Bakker kutoka Bayer Leverkusen, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa Magpies kwenye dirisha la Januari.

Tetesi zinasema, Tottenham wamekubali kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, kwenda Valencia.

Liverpool wamefanya mawasiliano na mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa miaka 28 ukikamilika msimu wa joto.

Matumaini ya Arsenal kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 25, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka Juventus yako mashakani. Miamba hao wa Serie A wanatafuta makubaliano ya miezi 18.

 

Tetesi zinasema, Arsenal wanatarajiwa kuimarisha harakati zao za kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa Mbrazil Douglas Luiz, 23, kabla ya dirisha la uhamisho kukamilika.

Tetesi zinasema, Leicester wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Angers mwenye umri wa miaka 18 Mohamed Ali-Cho, huku Mfaransa huyo pia akihusishwa na Tottenham.

West Ham na Crystal Palace wanatazamia kutaka kumnunua mshambuliaji wa Senegal na Marseille Bamba Dieng, 21, huku timu hiyo ya Ufaransa ikiwa tayari kumwachia mwezi huu kwa pauni milioni 8.

Tetesi zinasema, Brighton wameona ombi lao la kumnunua mshambuliaji wa Uhispania Abel Ruiz, 21, limekataliwa na Braga.

 


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe