Tetesi zinasema, Manchester United wanaweza kumnasa mchezaji wa Denmark Christian Eriksen kwa uhamisho huru kufuatia mkataba wake wa muda mfupi na Brentford kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni.

Arsenal wako tayari kumpa mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 25, mshahara wa wiki wa pauni 190,000 ili kuhamia Emirates Stadium msimu huu wa joto.

Liverpool wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua winga wa Leeds na Brazil Raphinha, 25, baada ya tetezi za kuondoka msimu huu kwa mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30, kuzidi kuongezeka.

 

Chelsea

Chelsea wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 25 ambaye atapatikana bure baada ya mkataba wake utakapokamilika mwezi Juni.

Tetesi zinasema, Meneja wa Roma Jose Mourinho, 59, ameibuka kuwa mpinzani wa Zinedine Zidane kuwania nafasi ya Mauricio Pochettino kama meneja wa Paris St-Germain.

Tetesi zinasema, Tottenham, Newcastle na Aston Villa zote zinamtaka winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco mwenye umri wa miaka 28 kutoka Atletico Madrid.

AC Milan na Juventus wanamfuatilia winga wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Christian Pulisic, ambaye hafurahishwi na kusugua benchi Stamford Bridge.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Tottenham wanavutiwa na mshambuliaji wa Newcastle mwenye umri wa miaka 25 na Mfaransa Allan Saint-Maximin.

Tetesi zinasema, Newcastle itahitaji kulipa pauni milioni 50 ili kumsajili beki wa Manchester City Mholanzi Nathan Ake, 27.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa