Nyota wa zamai wa Monaco Tiemoue Bakayoko ambaye ametumia msimu wake wa 2018/19 kwa kuwachezea AC Milan kwa mkopo ameweka bayana mapenzi yake ya kwenda kukipiga ufaransa. Nyota huyu anatarajiwa kurejea Chelsea kiangazi hiki wakati Milan wakionekana hawana mpango wa kumnunua moja kwa moja staa huyu.
Staa huyu bado ana mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Chelsea, klabu ambayo ipo katika joto la kuzuiwa kufanya usajili. Tiemoue Bakayoko anasema anatarajia kurejea Chelsea, lakini kiuhalisia angetamani kuwepo Paris.

Alipoulizwa kuhusu hatma yake, anasema kuwa asingependa kuficha jambo lolote. “Ni kweli siku moja natamani nicheze Paris. Siwezi kudanganya kuhusu hilo. Ni kitu kikubwa kwangu na wapendwa wangu. Sisi ni Waparisi wa kweli.”
Akizungumzia ndoto yake hiyo ya kuchezea PSG, anasema atarejea Chelsea kumalizia mda wake. Alifanikiwa kucheza mara kwa mara akiwa chini ya Gennaro Gattuso lakini anakiri kuwa mwanzoni alikuwa na wakati mgumu sana klabuni hapo. Staa huyu anasema hawakuwa na uhusiano mzuri na meneja Gattuso.


Zainabu
Aende tu
Rehema Dickson
Aende akatimize ndoto zake ni sawa kwa kila mtu kua namatamio na nafasi ikitokea unatakiwa uitumie ipasavyo
Povel
Aende mzee wa uchebe