Todibo Kwenda Man United Dili Lipo Palepale

Dili la beki wa klabu ya OGC Nice raia wa kimataifa wa Ufaransa Jean Claire Todibo kujiunga na klabu ya Manchester United linaelezwa bado halijafa na linafanyiwa kazi bado.

Ilisemekana huenda kusalia kwa beki Harry Maguire ndani ya Manchester United kungepelekea dili la Todibo kujiunga na Man United kufeli, Lakini taarifa zinaeleza bad mashetani wekundu wako kwenye mchakato wa kumsajili beki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa.tobidoKlabu ya Manchester United inaendelea na utaratibu wa kuwasiliana na klabu ya OGC Nice na kuangalia namna gani watawasilisha ofa yao juu ya beki huyo ambaye yupo kwenye orodha ya juu kabisa kati ya mabeki ambao wanawahitaji.

Kugoma kuondoka kwa Harry Maguire klabuni hapo na kujiunga na klabu ya West Ham kulipelekea dili hili kusimama kidogo, Lakini taarifa za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zinasema klabu hiyo bado inamuhitaji beki huyo.tobidoKlabu ya Manchester United inataka kuhakikisha inapata saini ya Todibo kwajili ya kuimarisha eneo la ulinzi la klabu hiyo, Kwani ni wazi kocha Erik Ten Hag hajamuweka Harry Maguire kwenye mipango yake na ndio sababu anahitaji beki mwingine wa katikati kwenye timu hiyo.

Acha ujumbe