Tumestahili Ushindi Dhidi ya Pep - Tuchel

Kocha Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema kuwa kikosi chake kilistahili ushindi dhidi ya Pep huku akitanabaisha kuwa Pep ni moja ya makocha bora Duniani.

Chelsea jana walipata ushindi wa 1-0 katika nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester City, goli la Hakim Ziyech kuifnaya Chelsea kutinga fainali huku akisubiri mshindi kati ya Leicester City au Southampton.

Tuchel
Hakim Ziyech na Timo

Kocha Thomas Tuchel kuhusu kama kumfunga Pep Guardiola kulikuwa kuna maana kubwa ya kudhihirisha mafanikio yake ndani ya Chelsea;“Unapocheza dhidi ya Pep Guardiola basi lazima ujue unacheza kwenye kiwango cha juu sana.”

“Guardiola amekuwa kocha wa timu za Barcelona, Bayern Munich na sasa yupo Man city, na ametengeneza alaka kubwa sana akiwa na timu zote na ata sasa ametengeneza alama kubwa ndani ya Ligi kuu Uingereza.”

“Lengo letu lilikuwa kupunguza pengo lolote ndani ya dakika 90 kwasababu kwenye soka lolote linaweza kutokea endapo ukicheza kwenye ubora unaotakiwa.”

Tuchel

Tuchel akaendelea kusema:“Nina furaha sana na najivunia kuhusu timu yangu ilivyocheza. Tumecheza kwa hari kubwa na kujiamini sana na tulikuwa na maarifa makubwa wakati tukiwa tunamiliki mpira na wakati tukiwa hatumiliki.”

“Tumestahili kupata ushindi dhidi ya labda kocha bora na bila ubishi dhidi ya moja kati ya klabu bora kwasasa. Tuna furaha sana kwa jinsi tulivyocheza na itakuwa sehemu kubwa kwetu kutupandisha juu kwenye kujiamini na kutupa motisha wa kuzidi kupambana.”


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Chelsea msimu huu wapo vinzur

    Jibu

    Pongezi kwa Chelsea

    Jibu

    Pongezi kwao chelsea

    Jibu

    Sema nini pep anajisikia sana

    Jibu

    Pongez zao chelsea

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.