Ule muda wa mashabiki wa soka kuanza kuburudika na mashindano ya Ligi ya Mabingwa (Uefa), umewadia! Timu bora barani Ulaya kuanza kupepetana wiki hii.
Baadhi ya timu zitakua na sura mpya kwenye vikosi vyao wakati vingine vikiwa kama vilivyokuwa msimu uliopita. Messi ndani ya PSG, Ronaldo ndani ya Man United, Grealish ndani ya Man City, Lukaku ndani ya Chelsea, Sabitzer ndani ya Bayern Munich, Alaba ndani ya Real Madrid na wengine wengi!!
Macho ya wengi yatakua pale Camp Nou ambapo Barcelona itawaalika Bayern Munich. Huu ni mchezo ambao Barca anaingia uwanjani akiwa na kumbukumbu ya kufungwa 8-2 na Bayern kwenye mashindano Uefa msimu uliopita. Kipigo kitaendelea au Bayern wataambulia patupu?

Liverpool atawaalika AC Milan pale Anfield. Hizi ni timu mbili zenye historia ya heshima kwenye mashindano haya. Milan watamkosa Zlatan Ibrahimovic ambaye amepata majeruhi, huku Liverpool wakimkosa chipukizi wao – Elliot ambaye naye ni majeruhi.

Inter Milan uso kwa uso na Real Madrid kwa mara nyingine msimu huu. Timu hizi zilikua kwenye kundi moja msimu uliopita na zimekutana tena msimu huu. Nani kuondoka na pointi 3 muhimu kwenye mchezo huu wa kwanza?
Mabingwa watetezi wa Uefa – Chelsea, watawaalika Zenit pale Stamford Bridge. Safari ya kutetea ubingwa inaanza rasmi!

Unaweza kutandaza tiketi yako ya ushindi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa kubashiri na Meridianbet. Bofya hapa kuingia mchezoni.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


