United: Upepo Wa Ten Hag Unavuma Kwa Kasi.

Wazungu wanaita “public opinion”, huku kwetu bongoland tunasema ni upepo/mtazamo wa jamii. Man United wapo kwenye nyakati hizi.

Amahakika, upepo wa kumsaka kocha mpya wa Manchester United unavuma kuelekea Uholanzi ambapo, Erik Ten Hag anatawala midomo, akili na matamanio ya mashabiki wa klabu hiyo.

Haijajulikana wazi ni nani atakayepewa mikoba ya kuiongoza klabu hiyo kuanzia msimu ujao lakini, Ten Hag na Pochettino wanatajwa kama fahali wawili wanaochuana vikali kwenye orodha ya kocha anayetarajiwa kule Old Trafford.

Pochettino anafaida ya uzoefu wa kuiongoza klabu ya inayocheza kwenye EPL. Ten Hag anasifika kwa uwezo wake wa kukuza wachezaji, kutengeneza kikosi/vikosi endelevu pamoja na kutwaa mataji. United hii inahitaji mabadiliko makubwa na, sehemu kubwa ya mashabiki wa klabu hiyo wanahitaji kuona uongozi wa timu hiyo ukitekeleza jukumu hilo kwa weledi na sio upendeleo na kujuana.

Richard Arnold.

The Red Devils sasa hivi wapo chini ya Richard Arnold kama Mkurugenzi mpya akichukua nafasi ya Ed Woodward ambaye kwa miaka 7 ameiongoza United bila mafanikio ndani ya uwanja.

Swali ni – Je, huu upepo wa Ten Hag utafanikiwa kumpatia nafasi Old Trafford au, uongozi wa klabu utaushangaza ulimwengu kwa kumpatia timu kocha tofauti ya Erik au Mauricio?


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe