Raisi wa FIFA Gianni Infantino amesema kuwa shirikisho hilo la mpira duniani halikuwa wazo lao la kutaka kuandaa michuano ya kombe la dunia kila baada ya miaka miwili lakini walikuwa wanafanya upembuzi yakinifu ya mabadiliko tu.
Wazo la kuandaa michuano hiyo kila baada ya miaka miaka miwili limepata upinzani mkubwa kutoka vyama vya soka mbalimbali, wachezaji na vionngozi wa ligi mbalimbali japokuwa chama cha soka Afrika ilikuwa inakubaliana na wazo hilo.
Awali rais Gianni Infantino alisema kuwa wote ambao walikuwa wanapinga wazo hilo alwaita waoga wa mabadiliko.
“FIFA haikundaa wazo la michuano ya kombe la dunia kuchezwa kila baada ya miaka miwili.” Infantino alisema
Infantino akizungumza mjini Doha kabla ya droo ya kupanga makundi ya timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kwenye majira ya baridi, aliendelea kusema, “ngoja tuweke mchakato sawa hapa, mkutano wa mwisho wa fifa uliomba uongozi wa fifam kufanya upembuzi yakinifu kuhusu mpango wa kuchezwa kwa mashindano hayo kila baada ya miaka miwili.
“Uongozi wa FIFA chini Arsene Wenger ndio ulifanya hivyo, Lakini FIFA haikutoa pendekezo lolote, lakini ilikuja kufanya hitimisho kwamba inawezekana, kwamba kama ungekuwa na athari.
“Tumekuta inawezekana na hata kuwa na matokeo mazuri kwa sehemu kubwa tu duniani, lakini pia kuna upinzani mkubwa kwenye hili na ndipo mjadara ulipoanzia.”
Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Wenger amekuwa akiipigia upatu wazo la kuchezwa kwa michuano hiyo kila baada ya miaka miwili kama sehemu ya kazi yake ya kiongozi wa maendeleo ya mpira duniani.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.