Man Utd Wamfanyia Mahojiano Mauricio Pochettino

Klabu ya Man Utd imafanyia mahojiano kocha wa klabu ya PSG Mauricio Pochettino wiki hii ili kuona kama anafaa kuqweza kubeba mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwisho wa msimu huu.

Wiki iliyopita klabu ya Man Utd walimfanyia mohajiano kocha wa klabu ya Ajax ili kuweza kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, kwa sasa bado kuna simtofahamu ya nani atakuwa kocha wa klabu hiyo licha  Erik ten Hag kupewa nafasi kubwa dhidi ya wengine.

Man Utd bado itaendelea kufanya mahojiano na makocha wengine ambao wataona kuwa nafasi hiyo wanaweza kuimudu, huku wahusika wanaofanya mahojiano hayo ni mkurugenzi wa michezo John Murtough na mkurugenzi wa ufundi Darren Fletcher, huku maamuzi ya mwisho yakitarajiwa kutolewa na Richard Arnold.

Mchakato wa kutafuta kocha mpya ambae atachukua majukumu ya kuinoa klabu hiyo yalianza mapema mwezi huu, kama majina yaliorodheshwa na sasa wamefika kwenye hatua ya kuwafanyia mahojiano.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe