Sergio Aguero alilazimika kustaafu kucheza mpira wa miguu kutokana na matatizo ya afya mwaka uliyopita lakini ameweza kuelezea mapenzi aliyonayo kwenye mchezo huo pendwa ulimwenguni na uwezekano wa kurejea kucheza tena.
Tatizo la moyo lilimfanya Aguero atangaze kutundika daluga akiwa na umri wa miaka 33 miezi michache baada ya kusajiliwa na Barcelona akitokea klabu ya Manchester City kwa uhamisho huru.
“Jana iliifunga akili yangu kwamba ninaweza kucheza tena soka,” Aguero aliiambia TyC Sport.
“Daktari aliniambia itanibidi nikae bila kucheza mpira kwa miezi mitano au sita lakini tayari nataka kuanza mazoezi tena.
“Nataka kucheza, nilialikwa Miami kucheza na sikwenda nataka kutuma ujumbe kwa dokta kwanza.”
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.