Kuelekea ufunguzi rasmi wa dirisha kubwa la usajili barani ulaya, Juni 9, 2021. Kylian Mbappe (PSG) na Erling Haaland (Borussia Dortmund), wanapasua vichwa vya mashabiki.

Imeripotiwa mara kadhaa kuwa Real Madrid inaziwinda sahihi za wachezaji hawa. Kipindi cha Zinedine Zidane, ilikuwa ni dhahiri Mbappe ndiye aliyekuwa mlengwa mkuu wa Madrid kwenye usajili wa dirisha kubwa mwaka huu.

Baada ya Zidane kuondoka na Carlo Ancelotti kukabidhiwa kijiti chake, haifahamiki kama Madrid bado wanampango na Mbappe. Yote 9, 10 ni kwamba, uongozi wa PSG hauna mpango wowote wa kumuuza Mbappe wala haitotokea mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru.

Usajili, Usajili, Mbappe na Haaland Pasua Vichwa., Meridianbet
Raisi wa PSG,Nasser Al-Khelaïfi (kushoto) akiwa na Kylian Mbappe (kulia)

Kwa mujibu wa raisi wa PSG, Nasser Al-Khelaïfi ameamua kuweka wazi msimamo wao kuwa “hatutokuja kumuuza Mbappe wala hatoondoka kama mchezaji huru. Ataendelea kubaki Paris, ni miongoni mwa wachezaji bora. Nina imani tutafikia makubaliano mazuri ya mkataba mpya.”

Kule Ujerumani, kama ilivyokuwa kwa Jadon Sancho msimu uliopita. Borussia Dortmund wameweka wazi dau lao litakalowafanya wafikirie kumuuza Erling Haaland majira haya ya kiangazi.

Usajili, Usajili, Mbappe na Haaland Pasua Vichwa., Meridianbet
Erling Haaland

BVB wameweka wazi, timu yeyote inayomtaka Haaland iwasilishe dau la pauni milioni 171. Tofauti na hapo, Haaland HAUZWI! Utofauti wa Haaland na Mbappe ni kwamba, ifikapo mwezi Juni, 2022 Haaland ataruhusiwa kuondoka BVB endapo timu inayomsajili itatoa dau la pauni milioni 75. Hii ni kulingana na makubaliano yake na BVB kwenye mkataba wake wa sasa.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa