PSG hawapo tayari kumuachia Kylian Mbappe. Tetesi za usajili za Real Madrid zimekuwa zikimtazama na kumuhusisha Mbappe na klabu hiyo.

Lakini, taarifa zinasema kuwa mipango ya uhamisho ya Real Madrid kwenye msimu ujao wa joto kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiathiriwa na mpango wa PSG kusalia na Kylian Mbappe.

Real walikuwa wanahusishwa na uhamisho wa gharama wa nyota huyu tangia dirisha la usajili lililopita. Taarifa za uhamisho wa Mbappe zimekuwa na sura ya tofauti mtaani hivi karibuni baada ya kuonekana kuna kusuasua katika makubaliano ya mkataba mpya.

Kylian Mbappe PSG

Mbappe kwa sasa amesalia na miezi 12 kwenye mkataba wake pale Parc de Princes, huku PSG bado wakiwa mbali na maafikiano ya kusaini mkataba mpya, hali inayopelekea kuwepo na minong’ono mingi juu ya hatma yake.

Hata hivyo, licha ya sintofahamu ya hatma ya staa huyu, raisi wa PSG Nasser Al-Khelaifi amethibitisha kuwa klabu inafanya kila iwezalo kumbakiza staa huyu.

“Ninahitaji kuweka sawa. Mbappe atasalia Paris, kamwe hatutamuuza, na kamwe hataondoka bure.” Nasser Al-Khelaifi


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa