Usiku wa Jana kulikuwa na mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya England dhidi ya Romania, huku kukiwa na mashabiki kadhaa uwanjani.

Mechi ilikuwa ya kibabe huku kila timu ikishambulia kwa wakati na mpaka dakika 90 zinakamilika ubao wa matokeo ulisomeka England 1 – Romania 0. Goli pekee la penati la Rashford ndio lililoamua mchezo huo.

Kitu kilichoteka hisia za watu wengi ni kitendo cha kapteni wa Uingereza, Jordan Henderson kukosa penati na kutoonekana kusumbuliwa na kitu hicho huku akijisifia kwamba amekosa penati nyingi tu sio hii pekee.

Calvert-Lewin alichezewa faulo ndani ya 18 lakini Henderson akataka kupiga badala ya Lewin mwenyewe na baada ya kuikosa hakuonekana kusumbuliwa kabisa. Mashabiki wengi walionekana kutoridhishwa na mchezaji huyo.

Baada ya mahojiano mechi ilipomalizika, mashabiki walionekana kukasirishwa na kitendo cha kuchukulia poa, kitendo ambacho mashabiki hao wanahisi ni kudharau mambo makubwa na kutotambua umuhimu wa jezi.

WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa