Van Dijk na Ramos, Mabeki Wagumu kwa Odegaard

Nyota wa Arsenal Martin Odegaard amebainisha kuwa beki wa Liverpool Virgil van Dijk ni mmoja kati ya walinzi wagumu zaidi ambao amewahi kukutana nao.

Staa huyu wa washika bunduki alicheza dakika zote 90 za mechi ya Norway dhidi ya Uholanzi, walikubali kichapo cha 2-0 wakikwama njiani kwenye safari yao ya kufuzu Kombe la Dunia.

Odegaard amewataka mabeki wagumu zaidi ambao amewahi kucheza dhidi yao. Staa huyu anamtaja Sergio Ramos na Virgil van Dijk kama mabeki wenaovuruga sana akili.

Odegaard anapata fursa ya kurejesha kisasi kwa Van Dijk Jumamosi ya wikiendi hii, Arsenal wanapokutana na Liverpool dimbani Anfield.

Nyota huyu, amecheza jumla ya gemu tisa za Ligi Kuu msimu huu, mechi tatu kati ya hizo akitokea Benchi.

Van Dijk na Ramos, Mabeki Wagumu kwa Odegaard
Martin Odegaard

Licha ya umri wake amekuwa na uzoefu mkubwa wa soka nchini Uholanzi, Hispania na Uingereza.

Baada ya kuwa kwenye fomu nzuri kwenye gemu nane zilizopita, Arsenal wanakutana na kibarua kigumu, zaidi dhidi ya Liverpool.

Akizungumzia uzoefu wake dhidi ya Virgil van Dijk na Ramos, Odegaard amenukuliwa akisema;

“Kimsingi ninaweza kumtaja Sergio Ramos, nimecheza dhidi yake mara kadhaa kule Hispania. Pia Virgil van Dijk, nimecheza dhidi yake nikiwa na timu ya taifa, ninaweza kusema hao wawili. Walikuwa wagumu sana”

Kwa mtazamo wa Odegaard, klabu yake Arsenal kwa sasa ipo kwenye muelekeo sahihi, na kesho yao inafurahisha. 😊


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe