Eden Hazard Ana Huzuni kwa Sasa - Martinez

Bosi wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez amekiri kuwa nyota wa kikosi chake kwa sasa ni mtu asiye na furaha linapokuja suala la soka.

Hazard bado hajaweza kuyafikia matarajio ya wengi klabuni Real Madrid, tangia alipokamilisha uhamisho wa pesa nyingi kutoka Chelsea.

Changamoto ya majeraha imekuwa ikiathiri kiwango cha nyota huyu, na hata alipokuwa poa alishindwa kufanya vizuri kama ambavyo ilikuwa inatarajiwa kwake.

Licha ya msimu huu kuwa katika hali yake nzuri kiafya, bado hajaweza kumshawishi meneja Carlo Ancelotti kumpa kipaumbele kwenye kikosi chake cha kwanza.

Van Dijk na Ramos, Mabeki Wagumu kwa Odegaard

Martinez aliamua kuzungumzia mtazamo wake juu ya hali ya Hazard kisoka kwa sasa, na akanukuliwa akisema;

“Tunahitaji afike Kombe la Dunia akiwa amejiandaa. Tumekuwa na kikosi kikubwa kwa sasa. Eden yupo katika kipindi cha mfadhaiko kwa upande wa soka.” – Martinez

Hazard kwa sasa anapambania kurejea kwenye ushawishi mkubwa dhidi ya meneja Ancelotti.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe