Van Persie Aendelea Kuaminiwa Feyenoord Licha Ya Kuzomewa

Uongozi wa klabu ya Feyenoord umefanya uamuzi muhimu kuhusu mustakabali wa kocha wao Robin van Persie baada ya kikao maalum cha bodi kufanyika kufuatia matokeo yasiyoridhisha. Gwiji huyo wa zamani wa Manchester United alikumbana na maneno makali kutoka kwa mashabiki kwenye mchezo dhidi ya NAC Breda walioambulia sare ya 3-3, matokeo yaliyoiacha Feyenoord ikiwa nyuma kwa pointi 19 dhidi ya vinara wa ligi PSV Eindhoven.

Van Persie Aendelea Kuaminiwa Feyenoord Licha ya Kuzomewa

Baada ya hali hiyo kuzua presha kubwa, viongozi wa klabu walikutana katika kile kilichoitwa “crunch summit” ili kujadili hatma ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 42. Hata hivyo, licha ya changamoto za msimu huu, uongozi wa Feyenoord umeamua kuendelea kumuamini Van Persie na kumpa muda zaidi kuiongoza timu katika kipindi hiki cha mpito.

Katika mechi hiyo dhidi ya NAC Breda, mashabiki waliimba maneno ya kumtaka aondoke, lakini Van Persie alionyesha utulivu na kusema amejifunza kuvumilia ukosoaji. Alieleza kuwa soka lina hisia nyingi kutoka kwa mashabiki, lakini maana ya kuwa shabiki ni kuisapoti timu katika nyakati nzuri na ngumu.

Van Persie Aendelea Kuaminiwa Feyenoord Licha ya Kuzomewa

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo pia alifananisha hali yake ya sasa na kipindi cha uchezaji wake alipokuwa akikumbana na ukosoaji mara kwa mara. Alisema uzoefu huo ulimfundisha kuwa na ngozi ngumu na kuendelea kupambana licha ya changamoto, akisisitiza kuwa bado anaamini katika falsafa yake ya kazi pamoja na uwezo wa kikosi chake.

Van Persie Aendelea Kuaminiwa Feyenoord Licha ya Kuzomewa

Ingawa ubingwa wa Eredivisie unaonekana kuwa mbali kwa sasa, Feyenoord bado wanapigania nafasi ya kufuzu UEFA Champions League. Wakiwa na mechi nane zilizobaki, Van Persie na kikosi chake watatafuta kumaliza msimu kwa nguvu, wakianza na mechi dhidi ya Excelsior Rotterdam kabla ya kukutana na AFC Ajax katika dabi kubwa ya Uholanzi inayojulikana kama De Klassieker.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.