Vifungo Ndani ya WWE

Kama ilivyo michezo yoyote ile duniani huwa na kanuni ambazo huongoza mashindano husika na pale unapotokea uvunjwaji wa kanuni hizo zilizowekwa basi hatua kali hutumika ili kurejesha heshima pale ilipoonekana kuwa na mapungufu. Na hilo ndilo linafanya mchezo wowote ule uheshimike kwa nafasi fulani.

Pamoja na kanuni hizo kuwekwa lakini bado kuna wapiganaji wengi wamezivunja wakiwa ulingoni jambo ambalo limewafanya wapewe adhabu na wengine kusimamishwa kabisa kujihusisha na mchezo huo kwa kipindi fulani.

Nyota waliowahi kukutana na makucha hayo ni:

Roman Reigns, ilikuwa ni kwenye WrestMania ya 31 ambapo nyota huyo alishindwa kujizuia na kuanzisha ugomvi mwingine kwa mpinzani wake na kusababisha vurugu hizo kuwaathiri kwa kiasi kikubwa mashabiki waliokuwa washiriki wakubwa ndani ya pambano lake hilo. Baada ya vurugu hizo na uvunjifu wa kanuni alifungiwa kwa siku 30.

Rob Van Dam, ni kati ya wapiganaji wenye majina makubwa sana ndani ya WWE na amepigana na majina makubwa sana kwenye historia yake akiwemo John Cena ambaye aliwahi kuonja kipigo cha RVD. Adhabu yake haikuwa ya ugomvi ila alikutwa na madawa ya kulevya ndani ya gari lake na kukutana na adhabu kali ya WWE ambao hawakubaliani na ishu hiyo kabisa.

Randy Orton, alikutana na adhabu ambayo ilihatarisha sana nafasi yake katika miaka ya 2012 ambapo ilitoa somo hata kwa kizazi cha sasa kinachoshiriki michuano hiyo ya WWE. Alikuwa ni mgomvi baada ya pigano kukamilika kwa tabia ya kuwafuata wapiganaji wenzake na kuwapiga nje ya ulingo. Adhabu yake ilikuwa ni kukaa nje siku 30.

Edge, hili lilikuwa pigo kubwa sana kwa kampuni lililokuwa linawasimamia nyota hao kutokana na kubainika kwamba walikuwa wanajihusisha na matumizi ya baadhi ya vitu ambavyo haviruhusiwi kisheria. Na adhabu hiyo iliwakumba nyota wengi wakubwa wakiwemo: Edge mwenyewe, Mr Kennedy, Randy Orton, William Regal, The Hurricane, Johnny Nitro ambao kwa kipindi chote ndiyo waliokuwa wapiganaji wenye majina makubwa.

Alberto Del Rio, tatizo ni lilelile la kuleta ugomvi nje ya ulingo, sakata ambalo ni kinyume kabisa na maadili ya nyota wote wa WWE, jambo hilo lilimpa adhabu ya kukaa nje kwa kipindi cha siku 30 bila malipo. Hilo liliathiri hata aliporejea kwenye viwango.

3 Komentara

    Namkubali sana mzee wa kuvizia

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.