Ulishawahi kujua viwanja vipi ni bora duniani vya soka Duniani? Unaweza kuwa ulifahamu baadhi ambavyo ulihisi ni bora zaidi. Hii hapa orodha ya viwanja bora duniani ambayo inakubaliwa na watu wengi.
10. Azadi Stadium – Iran

Hili ni dimba linalokamata nafasi ya kumi duniani kwa ukubwa. Unapatikana mjini Tehran -Iran na ulifunguliwa mwaka 1971, unatumiwa na vilabu vya Persepolis Tehran FC, Esteghlal Tehran FC. Uwanja huu una uwezo wa kuchukua mashabiki 78,116, na una sehemu kubwa zaidi yenye majengo ya huduma mbali mbali na nyumba.
9. San Siro – Italia

Huu ni uwanja mzuri unaopatikana Milan, Italia. Uwanja huu unaweza kufurahiwa na kila mtazamaji katika kila kona ya uwanja. Una uwezo wa kubeba watazamaji 80,000. Ndiyo uwanja uliotumiwa kwenye fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya 2020.
8. Anfield – Uingereza

Huu ni uwanja wa nyumbani wa Liverpool! Uwanja huu si mkubwa kwa idadi ya watu inayoweza kuwachukua ambayo ni 54,074. Unafahamika na kukubalika zidi kwa hali yake na mazingira ya uwanja na hadhi uliyojijengea ulaya.
7. Santiago Bernabeu – Hispania

Huu ni uwanja wa Real Madrid, unapatikana Hispania. Ni uwanja wenye historia ya kutumiwa na wachezaji wenye majina makubwa ambao wanauenzi kila uchwao. Christiano Ronaldo anautaja uwanja huu kama ‘nyumbani’!
6. Soccer City – South Africa

Uwanja huu mwanzo ulifahamika kama First National Bank Stadium, unapatikana jijini Johannesburg. Ulijingwa mwaka 2010 na una uwezo wa kubeba watu 90,000.
5. Azteca – Mexico

Ni uwanja ambao umekuwa maarufu zaidi kwa uwezo wake wa kubeba watazamaji wengi. Una uwezo wa kubeba watazamaji 100,000 na una heshima kubwa nchini Mexico.
4. Camp Nou – Hispania

Huu ndo uwanja mkubwa zaidi Hispania. Ni uwanja wa nyumbani wa Barcelona. Ni mmoja ya uwanja wenye heshima kubwa kwenye historia ya soka, Lionel Messi ni moja ya mastaa waliotumia uwanja huu kwa mda mrefu zaidi.
3. Old Trafford – Uingereza

Ni uwanja maarufu unaotumiwa na Manchester United kama uwanja wao wa nyumbani, moja ya klabu tajiri zaidi duniani. Unafahamika kwa jina jingine la “Theatre of Dreams” Uwanja huu upo nafasi ya 3 duniani.
2. The Allianz Arena – Ujerumani

Uwanja wa mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich! Una uwezo wa kuchukua watazamaji 70,000. Ni uwanja unaovutia sana nyakati za usiku ukipambwa na rangi nzuri, umeibuka kuwa uwanja wa pili kwa ubora duniani.
1. Wembley Football Stadium – Uingereza

Uwanja huu ulifunguliwa tena mwaka 2007 ukiwa umeboreshwa zaidi ya uwanja wa awali uliokuwepo eneo hilo hilo. Una uwezo wa kuchukua mashabiki 82,000
Unaweza kuwa ulivifahamu baadhi ya viwanja hapa na sasa unafahamu nafasi zake katika ubora wake kwa dunia nzima!


Omary lukumbi
Kusema kweli wenzetu wamewekeza sana kwa upande wa soka wana viwanja bomba na vya kisasa
Frank Patrick
Uingereza wametisha sana
Neema
Duuu hivo viwanja vizurii na vinavutia kwa macho ya watu wengi
Ester jackson
Jamani wameweza wezetu jamani sio kwa viwanja hivyo uingereza wametia fora
isha
Uingereza wako vizuri sana
Mwanahamisi
Hii ukweli kiwanja cha uingereza kipo vizuri
Amiri Kayera
Asant San kwanifumbua kujua
Tahiya
Duu wembley ni kiboko ina uwezo mkubwa kuliko viwanja vyote
Samiah
Uingereza wako vizuri
fatumakasomo
Uingereza wapo vizur
Mwanaidi
Kiwanja cha uingereza kipo vizuri zaidi
mwakalosi
Azteca ndio uwanja wangu number moja all time na ndio kiwanja pekee cha kwanza duniani kukifahamu
Antony Luseno
Kwangu namba moja ni Allianz arena kipo vizuri kimwonekano
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
Khadija
kwa kusema ukweli mnchi za wezetu wana viwanja vizuri tena vikubwa tena vinauwezo wa kuchukua idadi kubwa sana ya mashabiki kwa hapo bongo sijawahi kuona uwanja mkubwa kama wa san siro#meridianbettz
Zeiyana
San siro kiwanja kinamapato makubwa sana hadi imefikia kukalabati ili kizidi kuvutia zaidi ya pale mwanzo
Devotha
Hongera Africa ya kusini kwa kuwa na kiwanja bora
Rehema Dickson
ndio kiwanja pekee cha kwanza duniani chenye uzuri na mvuto wa pekee
Genia Sikaluzwe
Hongera Sana uingereza kwa kuwa na uwanja mzuri
felister
ahsanteni meridian bet nilikua silitambui hilo
Lydia Emmanuel Magoti
Mm kimuonekano Allianz arena kipo vizuri kimuonekano
Ester mmakasa
Aisee sisi tutasubiri kiukweli wenzetu wako vizuri na viwanja vyao.
Mariam mtandama
Safi
Elika
Camp nou imetulia sana japo kwa muonekano
Johnmary joel
Meridianbett asante kunifahamisha viwanja vya michezo nimevikubari ni vizuri sana#meridianbett
Caroline
Icho cha Italia sansiro..Ni kizuri jmn.
Dorophina
Nilikuwa sifahamu hiki kitu asante meridian kwa kunijuza
Samira
Uingereza wanakiwanja kizuri sana
Aziza mushi
Kiwanja kizuri Sana 👍
neema hassan
Asante kwa taarifa#meridianbettz
Rehema
Màana nilikuwa sijui hiki tu nashukuru sn meridianbet
Evaluziga
Hongereni kwa viwanja vizuri
Sadick
Nilifikiri Uwanja mpya wa Tottenham na Emirates vitakuwa kwenye orodha! Taarifa nzuri sana hizi#meridianbettz
Neema hassan
Asante kwa taarifa
Magdalena
Viwaja vyote ni vina muonekano mzur sana ila Cha South Africa ndo matata zaidi
Kenani
Kiwanja nmba 10 ndo kipo poa zaid
Issa
Hivi ni viwanja bora tunapaswa tuige na sisi kujenga pitch kama hizi
Njiku
Safii kwa taarifa ya viwanja vikali sana ila wembley ipo sana
Hamidu
Ningeshanga kama uwanja wa man utd usingetajwa…old Trafford mmoja wa viwanja bora duniani.#meridianbettz
Shafii
Nimewakubali Sana waingereza wameingiza viwanja vingi bora katika orodha ya viwanja vikari duniami
Christopher
Emirates upo wapi?
Furahav
Kiwanja chetu cha Taifa hakipo!!!
Salma
Uiengereza wametisha
Amani
Manchester United kama uwanja wao wa nyumbani, moja ya klabu tajiri zaidi duniani. Unafahamika kwa jina jingine la “Theatre of Dreams” zamani alikuwa panaitwa machinjioni ukiingia utoki # meridianbettz
Jullie
German wako vizuri
Theckla
Waingereza wapo vizuri Sana
Povel
Waingerezah Wana viwanja vzr sana
Hope mwaikuka
Dah! Nlkua cjui hili
Sabrina
Maoni:Asante sana kwa kunijuza #Meridianbettz
David Pere
Duuhhhhhh Yani Cha kwwtu hakipo kabisa hii kweli noma
Ernest
Mwandishi wa makala Hii ingefunguka pia na uwezo wa viwanja vingine katika kuchukua idadi ya watu tungefurahia zaidi makala hii
warda
Duuu uwanja wa Manchester ulitakiwa uwe wa kwanza#Meridianbettz
Salma
Uingereza wametisha
Theonestina
Uwanja mzur Sana huu.hongereni Sana uingereza
Asia Abdy
Kiwanja kizuri sanaa
Angelina
Daah ujeruman wako vizuri sana
Fatina mfingi
Makal nzur