Baadhi ya vitu shirikisho la soka duniani linavipinga kwa wanamichezo mengi ni kujihusisha na katika matumizi ya dawa za aina yoyote kwa wanamichezo wakiwa na lengo la kuzuia aina yoyote ya athari ambazo wahisika wangeweza kuzipata kwa kipindi fulani. Leo tunakuletea baadhi ya wachezaji waliopo na wengine wa miaka ya nyuma kidogo; ambao wameathirika [waliathirika] na madawa hayo kwa kiasi kikubwa pia waliojichanganya sana na starehe ya wanawake.
Garrincha
Mchezaji wa Brazil ambaye aliwika sana kabla ya akina Pelle kwa kunyanyua kombe la dunia miaka ya 1958 na 1962 kitu ambacho kilimpa heshima kubwa. Lakini aliweza kuangukia katika wimbi la matumizi ya madawa na kujihusisha sana na wanawake kitu ambacho kilimfanya aathirike sana kiafya na kuzidiwa nguvu na madawa hayo. Na kufikia mwaka 1983 aliweza kufariki kutokana na kasumba hiyo. Kutokana na kukutwa akiwa amepata madhara makubwa sana katika ini lake ambalo baadae lilishindwa kabisa kufanya kazi katika ufanisi wa kawaida.
George Best
Alikuwa mchezaji mkubwa ndani ya klabu ya Manchester United akiwa na historia kubwa ndani ya klabu hiyo. Japo pombe na madawa yaliweza kumwondoa kabisa kwenye ubora wake na kuanza kukumbana na maradhi ya mara kwa mara ambayo kwa kiasi kikubwa yalipelekea kuathirika kwa ini na baadae miaka ya 2005 aliweza kufariki kutokana na kuugulia kwa muda tatizo hilo. Kwa sababu miongoni mwa matatizo makubwa yanayotokana na matumizi ya vilevi vikali sana na madawa mara nyingi ni kuathirika kwa ini.
Diego Maradona
Anakumbukwa vitendo alivyovifanya akiwa katika kombe la dunia la Urusi mwaka 2018 kwa kulewa na kutumia vilevi vyake ambavyo vilimpelekea hata kuzuiwa na FIFA kuendelea kuhudhuria kuangalia mivhuamo hiyo kutokana na kuendeshwa sana na madawa hayo na kufanya vitendo ambavyo kwa heshima yake havikuwa sahihi sana kuvifanya kwa wakati ule. Pamoja na mapungufu hayo bado anabaki mchezaji wa kihistoria wa taifa hilo.
Mario Balotelli
Ni aina ya wachezaji watukutu kuwahi kutokea katika sayari hii kwa kiaka ya hivi karibuni. Ana uwezo wa pekee akitulia kucheza mpira lakini kuna wakati anapotea kabisa na kuonekana si chochote mbele ya wengine kutokana na vitendo vyake na nidhamu mbovu anayoionesha viwanjani na katika maisha yake ya kawaida. Kwa sasa amesaini na Olympique de Marseille kukiwa na makubaliano ya yeye kutokujihusisha na matumizi ya madawa ya aina yoyote pia vilevi vingine.


Ester jackson
Dash sikujua kama Diego maradona nae alikuwa mtukutu kiasi hicho mpaka kipelekea kutumia vilevi vya namna hiyo asante sana meridian
Njiku
Gud news