Wanamichezo Hawa Wapo Kama Hawapo Vile!

Siyo wanamichezo wote huwa maarufu kutokana na kile wanachokifanya. Wengine huwa maarufu kwa kipindi fulani tu lakini baada ya kutwaa tuzo hizo huweza kusahaulika hata ule uwepo wao; kwa maana kwamba wanakumbukwa baada ya matukio kinyume na hapo wanasahaulika kama wapo katika maisha yao kimichezo.

Huwa ni ndoto ya kila mwanamichezo kutengeneza historia ambayo ingeweza kumjenga na kumfanya yeye pia aweze kutengeneza kipato kikubwa kupitia umaarufu wake kama ilivyo kwa wanamichezo wengine kama Lewis, Ronaldo, Neymar, Messi hawa umaarufu wao unawapa fungu nono kwa ajili ya kutangaza biashara za wengine. Leo tunakuletea wana michezo wanaofanya vizuri lakini umaarufu wao ni wa matukio.

Andy Murray

Mchezaji mwenye wasifu mzuri kwenye tenisi akiwa na historia kubwa ya kuweza kufanya vizuri sana na ameweka historia nzuri ndani ya taifa hilo la Uingereza lakini linapokuja suala la kupata la kutumika kwa umaarufu wake ni miongoni mwa wanamichezo ambao hawatazamwi kwa jicho la pekee. Jambo hili linaanzia hata kwao kutokana na ile hali kwamba; endapo atashinda katika mechi au kikombe chochote basi huitwa Muingereza lakini akipoteza ataitwa Mscotland.

Justin Gatlin

Mwanariadha mwenye historia kubwa sana katika michuano mingi mikubwa. Amekuwa na historia kubwa aliyoijenga kwenye riadha lakini pamoja na mataji yake hajaweza kufahamika sana kama ilivyo kwa wenzake akina Bolt ambao wamefanya kitu kilichowajengea jina kubwa mbele ya mashabiki na mbele yao wao wenyewe na taifa lao. Mafanikio aliyoyapata mwaka 2017 mbele ya Bolt hayajampa kabisa ile heshima aliyostahili hadi leo.

Justin Gatlin
Justin Gatlin

Muhammad Ali

Alikuwa ni mwanamasumbwi mkubwa sana aliyeheshimiwa kwa kile alichokifanya katika kipindi chake chote cha kupanda ulingoni. Mara baada ya kuihama dini yake na kujiunga na Uislamu kulimfanya kusahaulika kabisa kwa kiwango kikubwa. Pia alichukiwa na wengi baada ya kugoma kushiriki kupambana katika vita dhidi ya Vietnam kukafanya watu kuacha kumfuatilia kwa kiwango kikubwa. Lakini baadaye akaanza kupendwa baada ya kufanya vizuri japo sio sana.

Floyd Mayweather

Ana rekodi ambayo haiwezi kulinganishwa kimafanikio na wapiganaji wengi wa sasa. Ameweza kucheza mapambano makubwa yanayotambulika mengi lakini ameshinda yoye 50-0 mbele ya wapinzani wake aliokutana nao ulingoni. Mbali na utajiri, mali na hata matokeo mazuri aliyo nayo hajawa mtu anayeuza sana mitandaoni bila kuwa na tukio linalomfanya ahusike.

2 Komentara

    Duh hii ni nouma Sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.