Soka ni mchezo wa ajabu sana ambao siku zote huibua mambo ya aina mbalimbali. Kuna wakati mchezaji huhama kutoka klabu moja kwenda nyingine kwa lengo la kubadili angalau mazingira lakini ili mchezaji yeyote asajiliwe klabu nyingine lazima aoneshe kiwango cha juu.
Kuna baadhi ya wachezaji hutoka klabu fulani na kujiunga na nyingine wakiwa katika kiwango cha juu sana lakini wanapojiunga na klabu nyingine hupotea. Suala hili mara nyingi huweza kuchangiwa na mifumo isiyo rafiki anayoenda kukutana nayo mchezaji huyo ndani ya klabu anayojiunga nayo.
Pia, jambo lingine ni aina ya wachezaji ambao mchezaji huyo anakutana nao kwenye timu husika ambao wanaweza kumpa ugumu wa kuendana na falsafa hizo. Baadhi ya watangulizi waliowahi kupoteza umakini kama huo ni ndani ya Madrid:
Asier Illaramendi
Mchezaji hatari kabisa ndani ya kikosi cha Real Sociedad aliyeshindwa kuwika akiwa na matajiri wa jiji la Madrid. Alionekana kama lulu sana mbele ya Madrid walipokuwa wanamfukuzia kitu ambacho walikuja kuhakiki kwamba biashara yao haikuwa sahihi kutokana na mchezaji huyo kushuka uwezo wake. Alitua kikosini hapo na kushindwa kupambana na Modric ambaye alionekana kuendana na hali ya kimfumo mapema.
Kaka
Jina kubwa sana masikioni mwa wapenda soka wengi duniani. Amekuwa mchezaji mkubwa ndani ya timu ya taifa na vikosi vya klabu nyingine alizozichezea. 2009 aliachana na AC Milan na kujiunga na Real Madrid ambako alipotea kabisa. Kutokana na hilo basi hakuonekana kama ni Kaka yule aliyekuwa anafahamika kiasi kile. Mechi zote 120 alizocheza zilionekana siyo kitu machoni kwa wengi kutokana na mategemeo.
Lassana Diarra
Amewachezea Madrid mechi 117 lakini hakuleta madhara ambayo wengi waliyategemea kutoka kwake. Baadhi ya klabu ambazo ameweza kuchezea na kuonesha madhara makubwa ni: Anzhi Makhachkala, Lokomotiv Moscow, Marseille, Al Jazira na PSG. Baada ya kipindi chote hicho alipotua Madrid akashindwa kabisa kuonesha makali yake.
Michael Owen
Amepita katika klabu mbalimbali na kuacha alama ambayo kiukweli haiwezi kufutika kabisa. Baadhi ya klabu hizo ni Newcastle United, Manchester United, Stoke City lakini alipotua Madrid alishindwa kabisa kuonesha makali yake na kufanikiwa kucheza mechi 45 na klabu hiyo.
Wengine walioshindwa kabisa kuwika ndani ya ardhi ya Bernabeu ni Jonathan Woodgate, Thomas Gravesen, Royston Drenthe, Klaas-Jan Huntelaar; hawa ni baadhi tu ya majina makubwa ambayo yalishindwa kudhihirisha ubora wao Bernabeu.


Mariam mtandama
Asante kwa taarifa meridianbet
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa # meridianbet