Washambuliaji Bora Kutoka Afrika

Bara la Afrika limekuwa na washambuliaji wafungaji mabao mahiri sana tangu enzi na enzi katika ligi mbalimbali duniani kote. Hata hivyo, kuna waliotisha zaidi ya wengine wote. Angalia hapa chini kuwafahamu: 

Inaendelea… 

George Weah

Rais wa sasa wa taifa la Liberia alikuwa anatisha sana katika soka la ulimwenguni enzi zake za ujana kabla hajashinda uchaguzi wa taifa lake mwaka 2017. Yeye ni mchezaji soka pekee wa Afrika ambaye ameshinda tuzo zote za FIFA World Player of the Year na ile tuzo nzuri sana na kubwa duniani, Ballon d’Or.

Alibarikiwa sana kuwa na kipaji na ujuzi wa soka na uwezo mkubwa sana wa kuona goli lilipo, kwa sasa ana umri wa miaka 53 na ameshinda medali nyingi sana akiwa na klabu mbalimbali na hata akiwa yeye binafsi.

Ukiachilia mbali suala la yeye kuwa ameshinda tuzo ya African Player of the Year mara tatu, Rais huyo wa Liberia alikuwa ndiye mfungaji bora kwa msimu wa 1994/1995 wa michuano ya Champions League.

Alishinda kombe la FA Cup akiwa na klabu ya soka ya Chelsea na lile la Ligue 1 akiwa na klabu ya soka ya Olympique Marseille.

Inasikitisha sana kuwa huyu Weah hakushinda lolote akiwa na taifa lake hilo. Ila hata hivyo bado anabakia kuwa ndiye moja ya washambuliaji wakubwa sana na walio bora kutoka Afrika.

Roger Milla

Roger Milla aliiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya 1990 World Cup kule nchini Italia na iliweka historia kubwa ambayo inadumu mpaka leo hii. Mcameroon huyo alikuwa na umri wa miaka 38 wakati alipoisaidia timu ya The Indomitable Lions kufunga mabao manne na kuweka historia ya kuwa ndiye mchezaji wa kwanza wa Afrika kufika hatua ya robo fainali.

Miaka minne mbele akiwa USA akafanikiwa kuwa ndiye anayeongoza katika ufungaji magoli akiwa na umri mkubwa zaidi ya wengine kwa wakati huo.

Mafanikio haya, hata hivyo, yalikuja mwishoni mwa soka lake la kimataifa. Kwa ujumla tunaweza sema kuwa alishinda mataji ya AFCON mara mbili, AFCON Golden Boot mara mbili na vile vile akawa ndiye Player of the Tournament mwaka 1986.

Tusisahau kuwa mkongwe huyu alitunukiwa kuwa ndiye African Player of the Year mara mbili, na pia CAF ikamtaja mara mbili kuwa ndiye Africa’s Player of the Century.

ITAENDELEA

45 Komentara

    Hii ni mpya kwangu nasubili muendelezo

    Jibu

    George weah ndo anafahamika kama king wa football afrika lakin watu kama Drogba ni zaidi mno

    Jibu

    Asante kwa taarifa nzuri sikujua kama kunawatu walikuwa na kipaji kikubwa na kufikia kuwa viongozi wanchi

    Jibu

    Roger Milla ajitahidii azidi kutuletea historia nzuri afrika ki mchezo

    Jibu

    Nihistoria nzr sanaa afrika kimchezo

    Jibu

    Makala nzuri nasubiri mwendelezo

    Jibu

    Africa ni bara lenye vipaji sana hasa vya mpira

    Jibu

    Asantee meridani kwa makala nzuri

    Jibu

    Bora umenijuza

    Jibu

    George weah Ni fundi mzuri wa mpira

    Jibu

    Kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo..

    Jibu

    habari nzuri kwa wapenzi wa soka

    Jibu

    Tupo pamoja meridian kwa makala zenu#meridianbettz

    Jibu

    Bonge la makala aiseee

    Jibu

    Pongezi kwao walitisha sana
    #meridianbettz

    Jibu

    Kwangu mimi George Weah anasitahili kudo. Mafanikio ktk ngazi ya Timu ya Taifa yanategemea mambo mengi ambayo mengi yalikuwa nje ya uwezo wake #meridianbettz

    Jibu

    Milla namkubali kitambo sana#Meridianbettz

    Jibu

    Makala nzuri Sana nasubiri mwendelezo.

    Jibu

    Afrika ni bara lenye vipaji vingi vya kila aina sio kwenye soka tuu.

    Jibu

    Ni makala nzur kwakwer najivunia kuwa mwafrika hakika kuna vipaji vingi sana hasa mpira

    Jibu

    Makala nzur

    Jibu

    George alitisha na Ndio mchezaji pekee duniani aliyeweka record ya kuchukua tuzo tatu kubwa kwa mwaka mmoja

    Jibu

    Afrika ni kituo cha wachezaji walio bora duniani isipokua shida ni ule uafrika wao

    Jibu

    Seeing is Believing….Drogba was the best to Me

    Jibu

    kwa leo Roger milla japo George weah anamafanikia zaid

    Jibu

    Roger Milla alikuwa mchezaji Babu kubwa na atari sana

    Jibu

    Africa tunavipaji sana sema msingi mzuri hatuna na bado wanatubania kwenye tuzo.

    Jibu

    Rogar miller namkubali sanaa

    Jibu

    Rogar Milla alikuwa mchezaji mzuri Sana jembe

    Jibu

    Wakal sana hao watu

    Jibu

    Makala nzuri Sana hii na subili muendelezo

    Jibu

    Africa tuna vipaji

    Jibu

    Asanteni meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Asante meridian kwa taarifa maana sikuwahi kuisikia

    Jibu

    Safi kabisa

    Jibu

    Makala nzuri ,Africa tuna vipaji vya pekee

    Jibu

    Tunajivunia wa Africa

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Bara la africa mungu karijaalia sana vipaji na watu wa kujituma kutumia vipaji vyao kama ajira hongerin sana sana

    Jibu

    Afrika mungu ametujalia vipaji na tunajua kivitumia

    Jibu

    George weah. Nakubali Sana

    Jibu

    Hao watu balaa

    Jibu

    Weah ni mtu mwenye bahati na mafanikio ni mfano wa kuigwa

    Jibu

    Roger Milla namkubali Sana Ila naisubiria mwendelezo

    Jibu

    Habari mjema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.