Watu watatu katika klabu ya FC Koln wamekutwa na maambukizi ya Corona, klabu hiyo imethibitisha japo wamesema mazoezi yataendelea kama ilivyopangwa. Koln ipo imebakiwa na mechi tisa na wapo nafasi ya kumi.
Bundesliga inatarajia kuwa Ligi ya kwanza Ulaya kurejea uwanjani.
Tarehe rasmi iliyotajwa ni tarehe 9 Mei lakini serikali imechelewa kufanya maamuzi ya kurejea hivyo kufanya tarehe kusogea hadi Mei 16 au 23.
Wale waliokutwa na virusi hawakuwa na dalili yoyote lakini watakaa karantini siki 15 imesema klabu.
“Wachezaji wote, makocha na watumishi wengine walipima Alhamis Covid-19,”
“FC Koln hawatataja majina kwa kuheshimu usiri wa walioathirika. Mazoezi yataendelea kama ilivyopangwa kwa kuzingatia taratibu zote za kuzuia maambukizi ambazo zimewekwa tangu April 6 kwenye mazoezi ya vikundi.
“Tumechukua hatua za kupima kikundi hicho tena, kama ushauri wa wataalamu wa afya ‘Taskforce Sports Medicine/Special Game Operation’ kutoka DFL.”
Alhamis, Chancellor Angela Merkel alisema maamuzi yoyote kuhusu lini shughuli za michezo zitarejea yatafanyika Jumatano Mei 6.
“Ni muhimu kutulia na kuheshimu taratibu za wataalamu wa afya,” alisema Merkel.
SADICK
Duh ukisia supu imetiwa nazi ndio hii!
samiah
Duuh unaweza onachongo ukazani kengeza hapo
Emmy cleopa
Ni muhimu kujua afya yako kwanza alafu mengine yanafuata, wapimwe ili wakianza wameanza
Zainabu
Hii Corona jamanii
Mathayo sonje
Mungu awape afya njema wapone haraka warejee kiwieanjani
furahav
Daah majanga.
wahida
Bora waanze tu lile joto la mazoez Corona atakimbia mwenyew
JULIANA
Sasa itakuaje jamani, Corona hiiii
Mwanaidi
Daaah mungu awaponye jmn
Aziza moshi
Duh !mungu awafanyie wepesi wapone na waweze kurejea uwanjan wakiwa na afya njema
WAZIRI SHOMARI
Mungu awafanyie wepesi wapone kwa halaka
Samira
Mungu awasaidie wapone haraka warejee uwanjani
Amani
Mungu awasaidie
Salma
Pole ya wachezaji waliokutwa na maambukizi
Hidaya Mohammed
Mwenyezi mungu awanusuru awape afya njema
Gabriel
🙏
Tahiya
Mambo yanazid kuwa magumu uko
Khadija
Mungu awasaidie wapone
Kenani
Mungu atulinde Mana hatuna ujanja
Schola
Tuombeane kwa kweli
isha
Duuh poleni sana