Wilfred Zaha Kutimkia Galatasaray

Mshambuliaji Wilfred Zaha ambaye alikua anaitumikia klabu ya Crystal Palace anakaribia kujiunga na klabu ya Galatasaray kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake kumalizika na Palace.

Mabingwa wa soka nchini Uturuki klabu ya Galatasaray wanaelezwa kufikia makubaliano na Wilfred Zaha kwajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 japo mpaka sasa dili hilo halijakamilika asilimia mia moja.wilfred zahaGalatasaray msimu ujao wanarejea kwenye ligi ya mabingwa ulaya hivo wanafanya sajili ambazo zitawaongezea ubora kwenye kikosi chao msimu ujao ili kufanya vizuri ligi ya mabingwa ulaya pamoja na kuteteta ubingwa wao nchini Uturuki.

Klabu ya Crystal Palace nao hawako nyuma kwani wameshampa ofa ya kusaini mkataba mpya Wilfred Zaha, Lakini inaonekana kama klabu ya Galatasaray wako mbele zaidi ya Palace na ofa yao ni nzuri zaidi huku mchezaji nao akionesha kila dalili atatimka.wilfred zahaWilfred Zaha ambaye amecheza ligi kuu ya Uingereza kwa muda mrefu anaona sasa ni wakati sahihi wa kuondoka ndani ya ligi hiyo na kuelekea nchi nyingine na moja kwa moja anatarajia kujiunga na mabingwa hao wa soka nchini Uturuki.

 

Acha ujumbe