Wiki kadhaa zilizopita kuna mambo yamekuwa yakizungumzwa ndani ya WWE kuhusu baadhi ya nyota wakiwemo Sasha Banks, Luke Harper, The Revival, Rusev, Anderson na Gallows ambayo yanawaweka kwenye wakati mgumu mno nyota hao wa mchezo huo wa mieleka wenye heshima.
Nyota wengi wanaonekana kutokuwa na furaha kabisa na waandaaji wa mchezo huo lakini wameamua kukaa kimya tu na wasizungumzie jambo hilo japo hata wao wenyewe linawatesa sana. Hiyo inatokana na kubadilika kwa uendeshaji wa mashindano hata namna muelekeo wa mashindano unavyoandaliwa.
Pamoja na kwamba walalamikaji wenyewe hawakutaka kufahamika ndani ya sakata hilo lakini fununu zimechomoza na sio jambo ambalo limekaa kama siri tena ila kuna watu tayari wameanza kugusiwa kwamba huenda ndiyo wahusika wakuu wakiwemo nyota watano wanaoshiriki michuano hiyo.
Shinsuke Nakamura, nyota huyo mwenye asili ya Japan amekuwa na historia nzuri aliyoijenga kimashindano miaka ya hivi karibuni lakini kutokana na kutotendewa haki pamoja na uwezo wake mkubwa ambao kuna wengi tu wanaoshiriki mashindano makubwa wanaukosa basi amekuwa mtu anayecheza SmackDown; kitu ambacjo kinatokana na kutokupewa nafasi ya kuwakilisha juu zaidi.
Chad Gable, miongoni mwa nyota wenye kiwango cha aina yake kuanzia alipokuwa ndani ya kundi la American Alpha lakini hata baada ya kuvunjika alionekana bado yupo imara kusimama kama mpiganaji na mwanamashindano mkubwa lakini kampuni lake linaonekana kutokumtendea vilivyo katika hali inayokubalika na kuendelea kusota kucheza ligi za chini ambazo kwa hakika sio za hadhi yake kabisa.
Cesaro, pamoja na uwezo wake wa kipekee bado anaendelea kuunganishwa katika timu kwenye mapambano yake lakini kwa uhalisia hata mwanamieleka yeyote akiulizwa juu ya nani anaweza kuwa na ushindani kutoka katika daraja hilo la chini kwa hakika jina la nyota huyo halitakosekana. Hata mechi yake na John Cena alionesha ufundi wa aina yake lakinj bado anaendelea kufunikwa ili aendelee kusota bila mafanikio.
Wengine ni mwanadada Mickie James na mnyama Ethan Carter au kwa jina jingine anafahamika kama EC3. Wote hawa wanastahili kupewa hadhi zao. Hata muonekano wake kwa hakika ni wa aina ya wachezaji wa mielekea kabisa. Ubunifu wake na mbinu za kupigana ni vitu ambavyo vinamfanya awe imara na mwenye uwezo; pia, mwanadada Mickie anastahili kabisa kuwa katika madaraja ya akina Asuka lakini hatendewi hivyo.


Issa
Ssfi kweli